Mugabe aonekana hadharani...Soma habari kamili na Matukio360..#share

Na Mashirika ya kimataifa
BAADA ya kuwekwa kizuizini kwa siku kadhaa na jeshi la Zimbabwe, Rais Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza akiwa katika mji mkuu Harare.

Rais Robert Mugabe
Rais Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi.
Jeshi limesema lilikuwa kwenye mazungumzo na rais huyo na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazungumzo hayo haraka iwezekanavyo.
Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kumfuta kazi Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua uongozi wa Zanu-PF na urais.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search