Takwimu: Asilimia 17 watoto huzaliwa njiti...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
TAKWIMU zinaonesha asilimia 13 hadi 17 ya watoto huzaliwa
njiti nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Kinga katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Janneth Mghamba akizungumza kwenye maadhimisho ya
mtoto Njiti Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 17 kila mwaka. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Hedwiga Swai.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamayila wakati wa maadhimisho ya siku
ya Kimataifa ya Watoto Njiti ambayo huadhimishwa Novemba 17 kila mwaka.
Amesema Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la vifo vya watoto wachanga walio chini
ya mwezi mmoja hivyo kutokana na hali hiyo serikali inapaswa kudhibiti vifo kwa
watoto wachanga.
“Serikali imeweka mikakati endeleveu ya
kupunguza vifo vya watoto njiti kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya
nchini,”amesema.
Amesema moja ya program hizo ni kumsaidia mtoto kupumua baada ya kuzaliwa, kupanua huduma za watoto wachanga kwa kujenga wodi za watoto wachanga katika hospitali za manispaa na wilaya pamoja na kutoa mafunzo kwa wa hudumu wa afya jinsi ya ya kuhudumia watoto wachanga.
No comments:
Post a Comment