Serikali kusimamia sera kulinda watoto ...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abrahama Ntambara
SERIKALI itaendelea kusimamia sera za kulinda
watoto ili kuhakikisha wanakuwa katika makuzi
mema hususani kwenye lishe,
elimu na dhidi ya vitendo vya ukatili.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu
wa Wizaya ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Ave Maria Semakafu alipokuwa
akifungua Mkutano wa Pili wa Kimataifa juu ya Maendeleo ya Watoto ulioandaliwa
na Taasisi ya Chuo Kikuu cha Aga Khan ya Maendeleo ya Binadamu (IHD) kwa
kushirikiana na Taasisi za The Conrad N. Hilton na Aga Khan.
Amesema pamoja na jitihada hizo za serikali, ametaka
kuwepo kwa ushirikiano baina ya serikali na wadau mbalimbali wakiwemo Mashirika
yasiyo ya kiserikali na jamii katika kulinda watoto.
“Tunatakiwa kushirikiana na kusaidiana kwa pamoja katika
kulinda haki za watoto,’’ amesema Semakafu.
Aidha ametaka mkutano huo uwe chachu ya kuja na mikakati
ambayo itaboresha mazingira ya watoto katika maeneo ya elimu, afya, lishe,
ukatili dhidi yao ili kuhakikisha changamoto zinazowakabili zinapatiwa
ufumbuzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya IHD Profesa. Kofi
Marfo, amesema kuwa kila mmoja anao wajibu kwa
maendeleo ya watoto ikiwa ni pamoja na
wazazi, familia, jamii na Taifa.
“Tuna jukumu la pamoja la kuhakikisha watoto wetu wanakua
katika mazingira salama, kama vile wakati wa kucheza, maji salama ya kunywa,
lishe bora, vituo vya afya na hospitali kwa ajili ya matibabu wakati wakiwa
wagonjwa na mengine zaidi,” amesema Prof. Marfo.
Naye Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Profesa Joe
Lugalla amesema mkutano huo utakuwa wa siku tatu unahusisha watifiti, wasomi na
watunga sera na watajadili maendeleo ya watoto kwa kutatua changamoto
zinazowakabili.
Nyingine ni kusimamia tabia zisizofaa za wanafunzi wenye ulemavu
wa utambuzi kabla ya usalama wa shule katika makazi yasiyo rasmi pamoja na
masomo ya kesi inayotolewa katika Afrika, India, China na Paksitan.
No comments:
Post a Comment