Utendaji wa waziri Lukuvi mhh!!!...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na mwandishi
wetu
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi ameelezea utendaji wake wa
miaka miwili tangu ateuliwe nafasi hiyo
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiongea wakati wa uzindua wa miradi ya upatikanaji wa picha za anga na mfumo unganishi wa menegiment ya taarifa za umma (ILMIS) jijini Dar es Salaam hivi karibuni
Amesema lengo
la Serikali ni kupima kila kipande cha ardhi nchini na hati za kimila 46,000 zimetolewa na Serikali
Mapato ya Serikali yameongezeka kutoka milioni 46 hadi
bilioni 100 kutokana na mifumo dhabiti ya ukusanyaji Kodi
Migogoro zaidi ya Elfu 30
imetatuliwa kati ya migogoro 62,529 iliyopokelewa Katika Mabaraza ya Ardhi
nchini.
Amesema muda wa kupata Hati
umepungua kutoka siku 90 hadi 30 tangu maombi kupokelewa
Makazi zaidi ya 20,040 yametambuliwa na kurasimishwa. Serikali
inakamilisha sera ya Ardhi iliyozingatia maoni ya wadau
Pia Serikali
imeunda kanda 8 ili kuongeza tija katika kuwahudumia wananchi.Wizara yake imenunua vifaa vipya na vya kisasa vya
upimaji ardhi ili kuboresha utendaji katika kanda ilizounda
Mashamba zaidi ya 150 yamefutiwa Hati kwa kuwa
hayakuwa yameendelezwa ili yatumike na wananchi
Kampuni 61 zimesajiliwa ili
kusaidia upimaji wa ardhi nchini na
kwamba kama umekopa fedha ili kuendeleza shamba lazima utumie kwa kusudi hilo
tu na si vinginevyo
Amesema wizara yake sasa imeanza
kujenga mifumo ya kielektroniki ili kudhibiti taarifa za ardhi na kuanzia
mwakani taarifa za ardhi zitakuwa katika mfumo wa kielektroniki utakaondoa
udanganyifu
Kanzi Data ya taarifa za ardhi
imeshajengwa na mfumo wa kielektroniki
utaunganishwa na mifumo ya NIDA
No comments:
Post a Comment