Wanaokufa kwa kisukari waongezeka...soma habari kamili na Matukio360..#share

Salha Mohamed
 IMEELEZWA ifikapo mwaka 2030 ugonjwa wa kisukari nchini unakadiriwa kusababisha vifo  vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza kwa asilimia 7.


Waziri, Ummy mwalimu

Makadirio hayo  yametolewa  jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa muungano wa vyama vya magonjwa yasiyoambukiza Tanzania(TANCDA), Tatizo Waane na kuwa kisukari ni ugonjwa unaokuwa kwa kasi duniani.

 Pia amesema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu anatarajia kuwa mgeni rasmi katika matembezi ya kujenga ufahamu wa uwepo wa ugonjwa wa kisukari nchini.

Matembezi hayo yatafanyika Novemba 11, 2017 ikiwa ni kuenzi siku ya kisukari duniani Novemba 14 ya kila mwaka.

"Kisukari ni moja wapo ya magonjwa yasiyoambukiza na kwas asa  huchangia asilimia mbili ya vifo vinavyosababishwa na magonjwa hayo. Lakini ifikapo mwaka 2030 makadirio ni asilimia 7 ya vifo nchini itatokana na kisukari "amesema.

Waane amesema matembezi hayo yatahamasisha watu kupambana na ugonjwa huo hatari duniani kwa kufanya mazoezi kama njia kuu ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Amesema matembezi hayo yataanzia kiwanja cha mpira cha chuo cha Muhimbili (Muhas),  kupitia barabara ya umoja wa mataifa kisha kupita barabara ya Morogoro na Lumumba na kumaliza viwanja vya mnazi mmoja.

" Mgeni rasmi atapata fursa a kuzungumzia ukubwa wa tatizo la kisukari nchini na changamoto zinazowapata watu wenye kisukari nchini, "amesema.

Kauli mbiu katika matembezi hayo ni 'Wanawake na kisukari, haki yetu kwa afya njema'.
           


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search