SUMATRA yapiga marufuku kuzungumza siasa, dini, biashara ndani ya basi ...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na mwandishiwetu
MAMLAKA YA
Usimamizi wausafri wanchikavu na majini (SUMATRA) imepiga marufuku abiria kuzungumza masuala ya siasa,
dini na kufanya biashara wawapo safarini.
Mabasi yaendayo mikoani
Agizo hilo limetangazwa jijini
Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuuwa Sumatra, Lingadi Ngewe na
kwamba abiria atakayebainika kufanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Agizo hilo linakuja baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwapo kwa mvutano wa kupinga kanuni mpya kati ya
Sumatra na chama cha wamiliki mabasi yaendayo mikoani (Taboa) na wausafiri Dar es Salaam (UWAMADAR).
Bila kutaja ni sheria
na kununi ipi Mkurugenzi huyo amesema ufanyaji wa vitendo hivyo katika mabasi ni kinyume
na kanuni za usafirishaji.
"Tutaanza kuzuia wasafiri wa wapo ndani ya mabasi kuacha kuzungumza masuala ya siasa,
dini na kufanya biashara. Tukibaini hilo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa abiria na dereva ikibidi," amesema
na kuongeza
‘Kwa madereva hasa wa kwenda mikoani,
njiani wanapandisha wafanyabiashara na kufanyabiashara ndani ya basi, hatua kali
zitachukuliwa kwa dereva na huyo anayefanyabiashara.’
Jana jijini Dar es
Salaa mpamoja na kukanusha kuwapo kwa mgomo, Taboa na Uwamadar wamedai kuwapo katika malumbano ya kanuni
na sheria mpya zinazotarajia kutumika hivi karibuni baada yamchakato wake kukamilika.
Mwenyekiti wa UWAMADAR,
Kismat Dhalla amesema pamoja na mambo mengine Jumatano wiki hii watakaa na Sumatra
kujadili masuala kadhaa ikiwamo kanuni na sheria mpya za usafirishaji.
Hata hivyo Mweka hazina wa Taboa,
Issa Nkya amesema wapo kwenye msuguano na Sumatra kuhusu kanuni na sheria hizo na
kwamba watazipatia ufumbuzi muda si mrefu.
Mkurugenzi wa huduma za sheria wa
Sumatra, Tumaini Silaa amesema Sumatra
ipo kwa ajili ya kuhakikisha wadau wote wa usafiri wanapata haki sawa.
Amesema sheria na
kanuni mpya bado zipo katika mchakato na kwamba haziwezi kuanza hadi hapo wadau wote watakapoku baliana.
‘Kimsingi mambo haya
ya kisheria na kanuni mpya haziwezi kuanza kabla ya kujadiliana na wadau wote wa usafiri,
hivyo naamini hili haliwezi kuwa jambo kubwa sana na litapatiwa mfumbuzi,’ amesema.
Siasa ndio maisha yenyewe, kwa hiyo wakae kimya km wanaenda msibani!
ReplyDelete