TFDA yazindua maabara hamishika, kudhibiti dawa duni...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abraham Ntambara
KATIKA juhudi za kudhibiti dawa duni na bandia nchini Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imezindua Maabara Hamishika (Minlab Kits) nyingine 10 zenye thamani ya sh. milioni 100 na kufanya idadi yake kuwa 25.
"Ongezeko la maabara hizi litaongeza idadi ya vituo vya uchunguzi na kuimarisha ufuatiliaji wa ubora wa dawa katika soko," amesema Sillo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimuwa, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maabara Hamisika (Minlab Kits) 10 zilizonunuliwa na TFDA jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa
TFDA Hiiti Sillo, amesema kununuliwa kwa maabara hizo kunatokana na mafanikio
yaliyokwisha patikana kupitia mpango huo na kwa lengo kuongeza idadi ya sampuli
za kuchunguza, ameeleza kila maabara imegharimu sh. milioni 10."Ongezeko la maabara hizi litaongeza idadi ya vituo vya uchunguzi na kuimarisha ufuatiliaji wa ubora wa dawa katika soko," amesema Sillo.
Aidha ameeleza kuwa hatua hiyo inadhihirisha
kwamba Mamlaka imejidhatiti katika kutekeleza majukumu yake ya kulinda afya ya
jamii dhidi ya madhara yatokenayo na matumizi ya dawa duni na bandia.
Abainisha kuwa maabara hizo
zitapelekwa katika ofisi tatu za kanda za TFDA ambazo ni Tabora (Magharibi),
Mbeya (Nyanda za Juu Kusini) na Mtwara (Kusini).
Amesema nyingine zitapelekwa
katika vituo vituo vya forodha vya Namangan a uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
KIA ( Kanda ya Kaskazini), Sirari na Mtukula (Kanda Mashariki) na nyingine zitapelekwa
katika hospitali za mikoa ya Geita na Katavi.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimuwa ameitaka Menejimenti ya Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) kuendelea kujenga uwezo wa wataalam wa maabara
wanaohusika na uchunguzi kupitia Maabara Hamishika (Minlab Kits) ili
kuendana na mabadiliko ya Sayansi na
Teknolojia.
“Naitaka Menejimenti ya TFDA iendelee
wataalamu wa maabara wanaohusika na uchunguzi kupitia maabara hizi ili kuendana
na mabad liko ya Sayansi na Teknolojia,” amesema Waziri Ummy.
Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maabara Hamishiki (Minlab Kits) jijini Dar es Salaam.
Aidha ameipongeza TFDA kwa kuendeleza
mpango wa uchunguzi wa awali wa dawa ulioanza mwaka 2012 katika baadhi ya
hospitali za Mikoa na Vituo vya forodha.
Amebainisha kuwa mpango huo unahusu
uchunguzi wa dawa muhimu za kifua kikuu, dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs),
dawa za malaria pamoja na vijidudu (antibiotics).
Waziri Ummy akizungumza kuhusu
maabara hizo, amesema ni hatua ambayo inalenga kuimarisha nguvu katika
uchunguzi wa haraka na wa awali wa dawa (preliminary screeming tests) na hivyo
kudhibiti ubora na usalama wa dawa zinazoingia nchini na zilizoko katika soko.
Amesema ni imani yake kuwa TFDA
itahakikisha kwamba maabara hizo zinapelekwa katika vituo vilivyopangwa na kutumika
kulingana na mpango wa ufuatiliaji wa ubora wa dawa nchini.
Aidha amewataka watakaozitumia
kuhakikisha wanazitumia kama ilivyokusudiwa ili ziweze kukaa muda mrefu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti Sillo akkizungumza wakati wa uzinduzi wa Maabara Hamishika jijini Dar es Salaam .
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipatiwa maelezo juu ya Maabara Hamishika.
No comments:
Post a Comment