400 wa chuo kikuu Dar es Salaam wajiunga CCM...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu
IKIWA ni muendelezo wa CCM
kuvuna wanachama wapya, leo katika viwanja vya shule ya msingi kibangu wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam takribani wanafunzi
400 wa shahada, stashahada na shahada za uzamivu wa chuo kikuu cha Dar es
Salaam(UDSM) wamejiunga na CCM.
Baadhi ya maafisa wa CCM kutoka makao makuu idara ya Itikadi na Uenezi, Shabani
Shabani na Saidi Saidi
Taarifa iliyotolewa na Idara
ya Itikadi na Uenezi wa CCM inasema katika mkutano wa ndani wa wanachama, uliyoratibiwa na viongozi wa
Umoja wa Vijana Tawi la Mabibo, ulihudhuriwa na maafisa wa CCM kutoka makao makuu
idara ya Itikadi na Uenezi, Shabani Shabani, Saidi Saidi na Debora Charles
ambaye anatokea Idara ya Siasa na
uhusiano wa Kimataifa, viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM seneti ya Mkoa wa Dar
es Salaam, Mwenyekiti wa serikali ya mtaa na
wanachama.
Mwenyekiti wa Tawi la Mabibo
Isack Ngombe amesema wanafunzi wa UDSM "Wasomi
kumuunga mkono rais Magufuli ni haki yao maana anafanyakazi nzuri, pia wanajiunga
na CCM kwa kuwa ndio Chama pekee kinachoshughulika na shida za wananchi
wanyonge".
Lakini pia amesema wapo
wanafunzi wengi zaidi wa chuo kikuu wangependa kujiunga na CCM hivyo ni jambo
la muda tu.
Maafisa kutoka makao makuu
ya CCM wamewakaribisha wanachama wapya wa CCM na kuwaasa, kuwa wamechagua chaguo
sahihi, wawe wanachama waaminifu wanaosadifu CCM MPYA na TanzaniaMpya kwa
kujitoa kusoma kwa bidii, kushirikiana na wenzao, kuwa mstari wa mbele kutimiza
wajibu wao na kutetea rasilimali za taifa letu.
Tangu kutangazwa mageuzi
makubwa kwa vitendo ndani ya CCM na
serikali yake wananchi wamakundi mbalimbali wamekuwa wakijiunga na CCM kwa
wingi wakiamini "CCM ni chama cha
siasa imara na ni daraja la kuwaunganisha watu na serikali walioichagua na
kuiunganisha serikali na watu inayotaka kuwahudumia."
No comments:
Post a Comment