CCM yaonya.....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimewaonya wanachama na viongozi wakati huu wa uchaguzi unaoendelea ndani ya chama katika ngazi ya mkoa na Jumuia zake kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni rais wa Tanzania, Dk John Magufuli.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imebaini kuwepo kwa minong'ono na tetesi za vitendo vya rushwa katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa chaguzi za Mwenyekiti, Mwenezi wa NEC na wote wanaoomba dhamana za uongozi katika jumuiya za chama. umoja wa vijana (UVCCM), umoja wa wanawake (UWT), na jumuiya ya wazazi (WAZAZI).
"Vitendo hivi havikubaliki, havivumiliki,na nikinyume na misingi, maadili na miiko ya Chama cha Mapinduzi ," imesema.


No comments:
Post a Comment