Mbunge Nassari avamiwa, risasi zalindima...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu.
MBUNGE wa Arumeru Mashariki (Chadema) Joshua Nassari usiku wa kuamkia leo amedai kuvamiwa na watu wenye silaha nyumbani kwake maeneo ya USA River.
Mbunge wa Arumeru mashariki Joshua Nassari akihutubia wananchi katika moja ya mikutano ya hadhara.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Nassari amedai watu hao walifyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba.
"Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha polisi," amesema.
Amedai kuwa amekuwa akitishiwa kuuawa kila siku na kwamba amekuwa hana amani ndani ya nchi yake.
No comments:
Post a Comment