Startimes kuonyesha'live' kombe la Dunia...soma habari kamili na matukio360..#share

Na Mwandishi Wetu

WAPENZI wa mpira wa miguu nchini jana walishuhudia matangazo ya moja kwa moja ya droo ya upangwaji wa hatua ya makundi ya kombe la dunia yatakayofanyika nchini Urusi mwaka 2018.
Mmoja wa wapenzi wa mpira wa miguu akipokea zawadi ya king'amuzi cha StarTimes kutoka kwa meneja uhusiano wa StarTimes Juma Suluhu baada ya kujibu swali linalohusu kombe la dunia katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya  Star Media (T) Ltd kwa kushirikiana na kampuni ya ubashiri wa matokeo ya michezo Princess Bet waliandaa hafla jijini Dar es Salaan iliyowawezesha wapenzi hao kushuhudia.

Katika hafla hiyo StarTimes walionyesha moja kwa moja (mbashara) droo ya upangaji wa makundi ya Kombe la Dunia ambayo ilikuwa ikifanyika jijini Moscow, Urusi.

Akizungumza katika hafla hiyo Meneja Uhusiano wa StarTimes Juma Suluhu alisema, “Tumejikita katika kuhakikisha kila mtanzania anaangalia taarifa, burudani na maudhui yote muhimu duniani ndio maana tunawwaletea kombe la dunia mpaka nyumbani. Hafla hii ya leo ni kielelezo tosha cha ninayoyasema”

“Sio rahisi kwa mtu kudhani kwamba watanzania wanaweza kuangalia hata droo ya kombe la dunia na kombe la dunia lenyewe kwa gharama nafuu kiasi hiki. Lakini ndio ukweli Kwamba StarTimes ndio mtoa huduma anayeelewa zaidi hali ya uchumi na kujaribu kuendana nayo”. aliongeza Juma.

Mbali na ushiriakiano huu wa StarTimes na Princess Bet kuonyesha mbashara droo ya Kombe la Dunia, StarTimes wataonyesha moja kwa moja matangazo ya michuano hiyo kutokea nchini Urusi.

"Kwa sasa tunayo ofa ya Krismasi kwa wateja wetu wote, tumepunguza bei ya king’amuzi chetu cha antenna kutoka 47,000 sasa kinapatikana kwa bei ya pungusho Tsh 34,000, yaani Kombe la Dunia kwa 34,000 Kweli? Pia tumepunguza bei ya Dikoda ya combo ambayo awali ilikuwa ikipatikana kwa Tsh 86,000 sasa itapatikana kwa 78,000 pekee kwa ambapo utapatiwa pamoja na Dish na kifurushi cha Mwezi mmoja Bure”.


“Burudani yote ya Krismasi, kombe la Dunia na mengine mengi kwa 34,000 pekee kwa sababu sisi ndio wafalme wa Burudani za Familia, msimu wa kukaa na familia utapendeza zaidi na StarTimes”, alisema.

Makundi hayo ni kima yanavyoonekana

Kundi A: Urusi, Saudi Arabia, Misri, Uruguay
Kundi B: Ureno, Uhispania, Morocco, Iran
Kundi C: Ufaransa, Australia, Peru, Denmark
Kundi D: Argentina, Croatia, Iceland, Nigeria
Kundi E: Brazil, Uswizi, Costa Rica, Serbia
Kundi F: Ujerumani , Mexico, Sweden, Korea Kusini
Kundi G: Ubelgiji , Panama, Tunisia, England
Kundi H: Poland, Senegal, Colombia, Japan.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search