Mbeya kwanza yaacha wachezaji saba...soma habari kamili na matukio360...#share
Yusta Nkwelengushe,Mbeya
MABOSI wa klabu
ya Mbeya kwanza ya jijini hapa umeamua
kuachana na wachezaji saba walioitumikia timu katika mzunguko wa kwanza wa ligi
daraja la kwanza kwa makosa ya utovu wa
nidhamu pamoja na kushuka kiwango.
Timu ya soka ya Mbeya kwanza
Kocha mkuu wa timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza
, Maka Mwalwisi amesema wachezaji hao walioachwa ni wale waliokuwa hawaonyeshi
juhudi za kuipigania timu ipate
mafanikio na kusonga mbele.
Amesema wachezaji wengi walioachwa ni wale waliosajiliwa kutoka mkoani Pwani na sasa
kikosi kinabaki na wachezaji 22 waliokuwepo tangu mwanzo wa msimu huu wa ligi .
Mwalwisi amesema ‘‘Nilijaribu kukaa nao ili
wajirekebishe lakini hilo lilishindikana na wale ambao viwango vilionekana
kushuka nilikuwa namfanyisha
mazoezi mmoja baada ya mwingine
nao nikaona ni mzigo tu.’’
Amesema wachezaji hao walioachwa pia walitaka kukwamisha safari yao ya kuipigania timu ili iweze kupanda daraja kutoka Ligi
daraja la kwanza hadi kushiriki Ligi Kuu
msimu ujao.
Baada ya kutoa taarifa kwa Mkurugenzi wa timu Batchu
Shiraz naye aliridhia na kuwaandikia barua za kuachana na timu yetu ili tupate
nafasi ya kuongeza wengine wazuri watakaoisaidia timu.
Katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo,Mbeya
kwanza imejipanga kuongeza nafasi za wachezaji wanne pekee ili kukamilisha
kikosi cha wachezaji 26 watakaoitumikia timu hiyo.
Nafasi wanazotarajia kusajili ni washambuliaji watatu
pamoja na kiungo ambao wataungana na
wenzao ili kuhakikisha timu inafanya vyema katika mechi zake tano ilizobakiwa
nazo.
No comments:
Post a Comment