Hivi hapa viwango vipya vya soka Duniani...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
Shirikisho la soka
Ulimwenguni FIFA limetoa viwango vipya vya soka duniani ambapo Tanzania imeshuka
kwa nafasi tano kutoka 120 hadi 125
Kikosi cha timu ya soka ya Ujerumani
Katika orodha hiyo sasa Ujerumani wamerudi tena kuchukua nafasi yao ya kwanza ambayo hapo mwanzo
ilienda kwa timu ya Brazil.
Brazil waliokuwa wakishika
nafasi ya kwanza sasa wamekuwa nafasi ya pili huku Ureno waliokuwa nafasi ya
sita sasa wako nafasi ya 3 na Argentina waliokuwa nafasi ya 3 wameshuka hadi 4.
Waliokuwa nafasi ya 3 wameshuka hadi 4.
Ubelgiji wamepanda hadi
nafasi ya 5 kutoka 9 walipokuwa huku nafasi ya 6 ikienda kwa Poland, timu ya
taifa ya Swiztrland wako katika nafasi ya 7 huku ya 8 ikikamatwa na Ufaransa.
Mabingwa wa Amerika Kusini
timu ya taifa ya Chile wako nafasi ya 9 huku wanaofunga orodha ya 10 bora ni
timu ya taifa kutoka bara la America timu ya Colombia.
Timu ya taifa ya Uingereza
ambayo imeshuka hadi nafasi ya 15 ikiwa ni baada ya miaka 17 kufika katika
hatua hiyo na wakipitwa na Wales walioko
13.
Kwa upande wa kumi bora ya
Africa, Misri wanaongoza wakifuatiwa na Tunisia huku Wasenegal wakiwa katika
nafasi ya 3, ya 4 ikienda kwa DRC.
Nigeria wako nafasi ya 5,
wakifuatiwa na mabingwa wa Africa timu ya taifa ya Cameroon huku Burkina Fasso
wakishika namba 7, 8 ni Ghana, 9 Ivory Coast na 10 ni Morocco.




No comments:
Post a Comment