Dk Shein asikitishwa!!!…soma habari kamili na matukio360..#share

Na Mwajuma Juma, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesikitishwa na idadi ndogo ya wageni wanojiunga katika idara ya kiswahili visiwani humo kujifunza lugha hiyo.

Pia amelitaka baraza la kiswahili Zanzibar (BAKIZA) kwa kushirikiana na chuo kikuu cha taifa Zabzibar (SUZA) waimarishe vipindi vya lugha ya Kiswahili kupitia redio na televisheni, ili kuongeza ubora wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohammed Shein kushoto akisalimiana na Prof,Alawiya Omar Swaleh mara baada ya kuwasili katika Uzinduzi wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  Zanzibar
Dk Shein ameyaeleza hayo leo katika hafla ya ufunguaji wa kongamano la kwanza la kimataifa la kiswahili linalofanyika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

"Sifurahishwa na uwepo wa idadi ndogo ya wageni wanaojiunga katika idara ya Kiswahili kujifunza lugha hii, nataka muongeze jitihada ili Zanzibar iendelee kuwa ni Oxford ya lugha ya Kiswahili duniani,’’ amesema Dk Shein

Amesema lugha ni sehemu ya utamaduni, hivyo jitihada zao za kukiendeleza Kiswahili ziende sambamba na juhudi zao za kuendeleza na kuihifadhi silka, mila, desturi na nyanja nyengine za utamaduni wao.
Amesema wazazi, walezi na walimu wana jukumu la kuhakikisha vijana wanalindwa dhidi ya athari zinazotokana na kuiga utamaduni wa nje na kuchangia katika kumomonyoka kwa maadili.

Dk Shein pia ameiagiza Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kuendeleza matamasha ya utamaduni kwa kuongeza ubunifu utakaosaidia kuongeza ubora na idadi ya watu hasa katika utalii.

“Si vibaya Wizara ikaandaa mafunzo hata ikiwa nje ya nchi, ili watu waone namna ambavyo wenzetu katika mataifa mengine wanavyofanya matamasha yao. Ni wazi kuwa kuona ni njia bora ya kujifunza, na sisi tuwe tayari tukajifunze kwa wale wanaofanya vizuri zaidi, ili matamasha yetu yawe mazuri zaidi”, amesema Dk. Shein.

Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Baraza la Kiswahili Zanzibar na kuhudhuriwa na watu kutoka mataifa mbali mbali yakiwemo Marekani, Ujerumani na Tanzania.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search