Kinana akubali yaishe CCM...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana
amekubali ombi la Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho la kumtaka kuendelea kumsaidia kwa nafasi
hiyo.
Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
Rais Magufuli ametoa ombi hilo akifungua mkutano mkuu wa CCM
taifa unaoendelea mjini Dodoma.
“Ni mshukuru mzee Kinana kwa kunisaidia sana katika kukiongoza
chama hiki na nimategemeo yangu ataendelea kunisaidia pia hapo baadae,” amesema Rais Magufuli.
Awali kulikuwa na minong’ono kuwa katika mkutano huu
angetangazwa katibu mkuu mwingine lakini kwa hatua hiyo ni kwamba inamaliza
uvumi huo.
Akiwasilisha agenda za mkutano huo Kinana amesema anakubali
ombi la mwenyekiti wake kwani kauli yake ni amri.
“Nashukuru kwa kuendelea kuniamini, tumekuwa tukiongea mara
nyingi mambo ya chama na yangu binafsi, lakini napogusia masuala yangu binafsi
amekuwa akisema nisubiri na kuniuliza nawasiwasi gani,” amesema Kinana.
Katibu mkuu huyo amemuahidi Rais Magufuli kuendelea kumsaidia
kazi hiyo ya kuleta mabadiliko katika chama kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment