Magufuli atoa msimamo wake...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es salaam
MWENYEKITI wa CCM, John Magufuli ametoa msimamo wake wa kiutendaji
kwa kipindi cha miaka mitano ijayo 2017-2022.
Mwenyekiti wa CCM, John Magufuli
Amesema mtendaji yoyote atayekwenda kinyume atashughulikiwa kwa
mujibu wa taratibu na kanuni za chama
hicho.
Msimamo huo ameutoa leo mjini Dodoma alipokuwa akifungua
mkutano mkuu wa CCM na kwamba mambo makuu manne ndio msingi na dira ya utendaji
katika chama hicho.
Magufuli ambaye pia ni
rais ameyataja mambo hayo kuwa ni kuimarisha CCM kwa kuongeza idadi ya
wanachama wa uhakika.
Kuhakikisha chama kinajitegemea kiuchumi na ni aibu kwa chama kuwa tegemezi.
Viongozi wa CCM kuwa
kiungo kati ya wananchi na serikali.
“Na ya nne ni viongozi
kuwa waadilifu na mfano kwa wananchi,” amesema Magufuli na kuongeza “Mkutano huu ukiridhia ndio malengo makuu ya mradi wa awamu ya nne ya kujenga na kukiimarisha
chama chetu.”
No comments:
Post a Comment