Kocha Hemed Moroko ataka Zanzibar Heroes isivunjwe...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar
Heroes’ Hemed Moroko ametakatimu hiyo isivunjwe, iendelezwe na kwamba itakuwa timu bora katika
mashindano yajayo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud akimvisha shada la maua kocha mkuu wa Zanzibar Heroes, Hemed Moroko mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar na Timu yake ikitokea Kenya Katika mashindano ya CECAFA CHALLENGE CUP.
“Kama ambavyo nilivyosema mwanzo, kuwa timu hii
unaweza kuiona ni ndogo lakini kwa sasa sio ndogo, lakini changamoto wahusika
wameweza kuziona na mimi katika ripoti yangu naweza kutoa ripoti kuwa iendelee kuwepo
kwa kufanya mazoezi kila baada ya muda”, amesema Moroko
Ameyasema hayo mara
baada ya kuwasili visiwani
Zanzibar wakitokea nchini Kenya.
Moroko amesema licha ya changamoto walizopata wakati
wa kuiandaa timu hiyo walipofika huko walitulia na kutafuta njia ya kuweza
kujipanga ili waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo.
“Kulikuwa na changamoto wakati tulipoondoka hadi
tulipofika lakini zilipunguwa na kuweza kujipanga vizuri hadi kufikia hatua hii
ya fainali”, alisema Moroko.
Nao wachezaji wa
timu hiyo wamesema mashindano
yalikuwa magumu.
Mlinzi wa timu hiyo Issa Haidar Mwalala amesema haikuwa
kazi rahisi kufikia hatua ya fainali kwa kuwa mashindano hayo yalijaa wachezaji
bora kutoka timu nyingine.
“Sisi hatukuwa na wachezaji
professional kama walivyo wenzetu lakini tulifanyakazi kubwa hadi kufikia hatua
hii”, amesema.
Ametaja sababu ya umoja, ushirikiano
na nidhamu kuwa uliwapa nguvu hadi kufikia hatua waliyofikia.
Pia siri nyingine ya mafanikio hadi timu kufikia hatua ya fainali
ni kujipanga na kutulia wakati wanapocheza mpira.
No comments:
Post a Comment