Sheikh Ponda aibwaga serikali...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abdulrahim Sadiki
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imeamuachia huru Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda katika rufaa iliyokatwa na
Jamuhuri kupinga Hukumu ya Mahakama ya Morogoro iliyomuachia huru Ponda.
Sheikh Issa Ponda
Sheikh Ponda ameachiwa huru
mbele ya Jaji Johnson Mkasimongwa ambaye amesema anakubaliana na uamuzi wa
Mahakama ya Morogoro kumuachia huru Sheikh Ponda katika kesi ya kutoa matamshi
ya uchochezi.
"Mahakama ya Morogoro
haikukosea kumuachia huru Sheikh Ponda na mimi nakubaliana na uamuzi huo, hivyo
namuachia huru,".
Miongoni mwa hoja alizozitoa
Jaji Mkasimongwa ni kwamba upande Jamhuri haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa
kosa lile la kuvunja amri ya Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe
katika mahakama hiyo ili imchukulie hatua zaidi.
Katika mashtaka yaliyokuwa
yakimkabiri katika Mahakama ya Morogoro, Sheikh Ponda anadaiwa August 10, 2013,
katika eneo la Uwanja wa Ndege, Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu
wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa
zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.
Pia inadaiwa aliwaagiza
waumini hao kuwa endapo watu hao watajitokeza kwao na kujitabulisha kwamba ni
kamati za ulinzi na usalama za misikiti, wafunge milango na madirisha wawapige.
Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni
kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu
Victoria Nongwa May 9, 2010, ambayo ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima
kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.
Kosa jingine inadaiwa August 10, 2013 katika eneo la Uwanja wa
Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi Mtwara
kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili kuwaua, kuwabaka na
kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni Waislamu.
No comments:
Post a Comment