Magufuli, Dk Shein, Mangula wachaguliwa tena...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dodoma
MKUTANO wa halmashauri kuu ya CCM(NEC) leo imemteua rais John Magufuli kugombea nafasi ya mwenyekiti wa
chama hicho taifa, Dk Shein makamu mwenyekiti Zanzibar na Mangula Makamu Mwenyekiti Bara.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na uenezi wa
chama hicho Humphrey Polepole kikao
hicho kimefikia uamuzi huo baada ya kutafakari kwa kina na kwa kuzingatia mwelekeo
mpya wa CCM. Awali kabla ya Nec. Kikao
cha kamati kuu(CC) kilitangulia.
Pia amesema mkutano mkuu wa CCM utafanyika Desemba 18 na 19, 2017 ili kuwapitisha
viongozi hao rasmi watakaongoza hadi mwaka 2022.
No comments:
Post a Comment