Sintofahamu yatawala Takukuru kumkamata Mchechu wa NHC...soma habari kamili na matukio360..#share


Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
TAARIFA zilizosambaa kuanzia mchana wa hii leo Jumapili ni  kwamba aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la nyumba(NHC) kabla ya kusimamishwa hapo jana,  Nehemiah Mchechu amekamatwa na  TAKUKURU kwa mahojiano.

Nehemiah Mchechu

Taarifa  hizo zinadai Jumanne ijayo  atafikishwa mahakamani  kujibu makosa ya Uhujumu Uchumi, Uchepushaji na matumizi mabaya ya madaraka.

Hata  hivyo ili kuthibitisha taarifa hizo matukio360 aliwatafuta baadhi ya watendaji wa Takukuru akiwamo  mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo   Valentino Mlowola ambaye amesema ;  "Siwezi kuzungumza chochote mtafute msemaji wa Takukuru, Pia kumbuka leo ni Jumapili nipo katika ibada hivyo sipo katika nafasi nzuri ya kuzunguma hayo labda kesho  Jumatatu.’’

Matukio360 ilipomtafuta Tunu Mleli ambaye andiye anayefahamika kama msemaji wa Takukuru alijibu ; "Samahani mtafute msemaji wa Takukuru na kutoa namba za huyo aliyedai kuwa msemaji. Pia namba hizo zilipopigwa  hazikupatikana.’’


Jana waziri wa Ardhi, Nyumba  na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alitangaza kumsimamisha Mchechu kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha na ofisi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search