Magufuli : NHC ijitathimini, inamadudu...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Dodoma
RAIS John Magufuli amelitaka
shirika la nyumba(NHC) kujitathimini
kutokana na matumizi yake ya kifedha na kwamba inamadudu.
Pia ametishia kuivunja bodi ya shirika hilo kama itaendelea na misuguano ya chini kwa chini.
Rais John Magufuli
Ametoa agizo hilo leo mjini
Dodoma alipokuwa akifungua nyumba za makazi za Iyumbu Dodoma na kwamba serikali
itakuwa tayari kuizamini NHC kukopa fedha bilioni 200 kuendeleza miradi nchini.
Amesema watendaji wa NHC
wanamisuguano ya ndani kwa maslahi binafsi ikiwamo kutaka nafasi ya mtendaji
mkuu wa shirika hilo, Nehemia Mchechu na kuwa mingine inachochewa na wanasiasa.
‘’Waziri wa ardhi, bodi ya
NHC na wakurugenzi mkae na kujitathimini kuhusu mwenendo mzima wa matumizi ya
fedha za NHC. Mkirekebisha hilo nitakuwa tayari kusaini na kulizamini shirika kukopa
fedha kuendeleza miradi mbalimbali,’’ amesema Magufuli.
Rais Magufuli amesema pamoja
na kazi nzuri inayofanywa na NHC lakini bado kuna ‘madudu’ matumizi mabaya ya kifedha katika
baadhi ya miradi na kuuelezea mradi wa Kawe jijini Dar es salaam.
‘’Mradi wa Kawe jijini Dar
es Salaam una ‘madudu’ najua mradi unaubia na mwekezaji wa nusu kwa nusu, mtu
mwenyewe namjua. Ukikamilika anaweza kudai fidia yoyote, anaweza hata kwenda
mahakamani,’’ amesema
Amesema ni vigumu kwake
kusaini fedha wa watanzania kwa ajili ya matumizi mabovu.
Mradi huo wa Iyumbu hadi leo takribani nyumba 150,000 zimekamilika na utakuwa na nyumba 300,000
Awali waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema NHC inatarajia kujenga kiwanda cha kuzalisha bati.
Awali waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema NHC inatarajia kujenga kiwanda cha kuzalisha bati.
No comments:
Post a Comment