Mwakyembe atoa msimamo kwa vilabu vya soka....soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
SERIKALI imevitaka vilabu vya mpira wa miguu nchini
vilivyoanzishwa kwa mfumo wa wananchama vinavyotaka kubadili mfumo wa kiuenedeshaji wa hisa kutenga
asilimia 51 kwa ajili ya wananchama na 49 kwa ajili ya mnunuzi.
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imekuja ikiwa hivi karibuni klabu ya Simba
ilifanya mabadiliko ya umiliki wa timu kuwa katika mfumo wa hisa na bilionea
Mohammed Dewji akishinda uwekezaji wa klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema lengo ni kulida asili na historia
ya vilabu husika.
“Haya ni matakwa ya kanuni za sheria la baraza la michezo la
taifa (BMT) (marekebisho) ya mwaka 2017 ambazo zinasomwa kwa moja na kanuni za
sheria za BMT za mwaka 1999, ambazo katika kanuni hizo zitaitwa kanuni kuu,”
amesema Dk. Mwakyembe.
Ufafanuzi wa kanuni
Kanuni kuu zinarekebishwa
kwa kuongeza mara baada ya kanuni ya 18, kanuni mpya ya 18A kama ifuatavyo..
Uuzwaji wa hisa vilabu vya michezo katika
kanuni ya 18A,-(1) Vyama au vilabu vya michezo vilivyoanzishwa na wanachama vikiamua kuuza
hisa zake vinapaswa kutenga asilimia 51 kwa ajili ya wananchama wake na
asilimia 49 kwa wanaotaka kununua.
(2) Katika kusimamia utekelezaji wa kifungu cha (1) cha
kanuni hii, chama cha kitaifa kinachosimamia mchezo husika kinapaswa
kutengeneza mwongozo wa muundo wa vilabu hivyo kwa mtindo wa hisa.
(3) Maombi ya uuzaji wa ununuzi wa hisa yatalazimika
yaidhinishwe na chombo husika kinachosimamia mitaji na dhamana kwa mujibu wa
sheria za nchi.
(4) Wakati wa kuuza hisa, vyama au vilabu vya michezo
vilivyoanzishwa na wanachama vitalazimika kuwa na azimio na kwamba
watakaoruhusiwa kununua hisa ni wanachama waliohakikiwa na klabu husika kupitia
taratibu zilizowekwa kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na uwazi.
Waziri Mwakyembe amesisitiza kuwa lengo
lakuzungumzia suala hilo si kwa ajili ya klabu ya Simba na Mohammed Dewji kwa
kufanya mabadiliko ya kimfumo lakini ametaka kuzingatiwa kwa kanuni na taratibu
za nchi.
No comments:
Post a Comment