Majaliwa akagua makazi ya makamu wa rais Dodoma..soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu
WAZIRI mkuu, Kassim Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa na makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan pindi atakapohamia Dodoma.
WAZIRI mkuu, Kassim Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa na makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan pindi atakapohamia Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Amefanya ukaguzi huo leo katika eneo la Kilimani, mjini Dodoma ambako yalikuwa makazi ya Mkuu wa Mkoa
huo.
Akitoa
taarifa ya ujenzi huo, Waziri wa Nchi (OWM) anayeshughulikia Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Ajira, Wenye Ulemavu na Vijana Jenista Mhagama alisema
Kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma kilibaini kuwa mahali
alipokuwa akiishi awali siyo sahihi kwa ajili ya makazi ya kudumu ya Mhe.
Makamu wa Rais.
“Pale palikuwa panafaa kwa ajili
ya ziara za kikazi alipokuwa akija Dodoma, kwa hiyo tumeamua tufanye ukarabati
hapa, ili aweze kuishi kwa viwango vinavyostahili.”
Alisema kazi ya matengenezo
kwenye makazi yake itagharimu sh. bilioni 1.5 wakati kazi ya kutenganisha ofisi
za watumishi na wasaidizi wa Makamu wa Rais itagharimu sh. milioni 680.
Waziri Mkuu pia alikagua
matengenezo ya Ofisi inayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais ambayo itakuwa
eneo la Ndejengwa.
Wakati huohuo, Kaimu
Meneja wa TBA Mkoa wa Dodoma, Bw. Steven Simba ambaye anasimamia ujenzi huo,
alimweleza Waziri Mkuu wanataraji kuwa kazi hiyo itakamilika kabla ya Desemba
30, mwaka huu.




No comments:
Post a Comment