TFDA kununua mitambo kudhibiti sumu kuvu...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) ipo katika mikakati ya kupata mitambo ya kisasa ya kuchunguza sumu kuvu ili kulinda afya za watumiaji wa nafaka hasa mahindi.
Sumu kuvu ni aina ya kemikali za sumu inayozalisha ukungu au
fangasi kwenye mbegu za nafaka kama mahindi, kunde na karanga.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa TFDA, Hiit Silo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kufunga mkutano wa siku mbili uliwakutanisha wataalam kutoka nchi 15 za Afrika.
Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kujadili mikakati ya
kudhibiti sumu kuvu katika nafaka.
“Kwa sababu kama ambavyo taarifa za nyuma zimetolewa ni
kwamba huwezi kutazama mahindi na kusema kwamba yana sumu kuvu lazima uwe na
uwezo wa kuchunguza,” amesema Sillo.
Sillo amesema kutokana na athari za sumu kuvu kwa afya ya
binadamu, TFDA imechukua hatua mbali mbali ya kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu madhara na umuhimu wa kutunza mahindi ili kuepukana na maradhi
yatokanayo na tatizo hilo.
Mkurugenzi wa usalama wa chakula wa TFDA, Raymond
Wigenge ameanisha mambo manne yanayotegenezewa miradi kwa ajili ya utekelezaji.
Mambo hayo ni uelimishaji jamii, teknolojia,
tafiti mbalimbali, na sera mahususi zinazolenga kushughulikia tatizo.
Wigenge amesema mazingira yenye unyevunyevu ni
rahisi kuzalisha fangasi wanaosababisha t sumu kuvu na amewataka wananchi kuhifadhi nafaka katika mazingira makavu.




No comments:
Post a Comment