Makalla akabidhi mabati 154, mifuko ya saruji 100....soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Mbeya
SERIKALI mkoani Mbeya imetoa
msaada wa mabati 154 na mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya milioni 4 katika zahanati ya kata ya Mwasanga na ujenzi wa kituo cha afya Iduda.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kushoto) akikabidhi mabati na mifuko ya seruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati na kituo cha afya mkoani humo
Akikabidhi msaada huo leo
mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla amesema mpango mkakati wa serikali ya mkoa ni
kuchangia vituo vya afya na zahanati zilizojengwa kwa nguvu ya wananchi.
Pia wakati ujenzi huo
ukiendelea ameagiza uongozi wa
halmashauri ya jiji kuboresha
miundombinu ya barabara.
"Huu ni mpango mkakati
wa mkoa katika kuchangia kila kata na
kijiji ambavyo vimethubutu kujenga vituo vya afya na zahanati na
sitoishia hapo nitahahakisha pindi vinapokamilika kunakuwepo na madaktari na wauguzi,"amesema.
Makalla amesema Serikali ya
viwanda haitoweze kufanikiwa ikiwa wananchi wanakosa huduma za msingi za maji, miundombinu ya barabara na huduma za afya hususan kwa wanaoishi pembezoni mwa mji.
Ameonya watendaji na wanasiasa
kutoingiza maslahi binafsi katika msaada huo na ametaka wananchi washirikishwe katika kila hatua ili
kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza katika miradi hiyo.
Diwani wa kata Mwasanga, Joe
Hokola amesema wananchi wamechangia milioni 1.2 za ununuzi wa vifaa mbalimbali
katika zahanati.
Mkazi wa Mwasanga, Sophia
Mumbonege amesema ujenzi wa kituo hicho cha
afya na zahanati kitawezesha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa kupunguza msongamano katika Hospitali ya mkoa wa Mbeya
No comments:
Post a Comment