Ukawa ‘kususia’ uchaguzi wa ubunge, udiwani....soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Dar es
Salaam
VYAMA vya siasa vinavyounda
umoja wa katiba(Ukawa) vimetaka uchaguzi wa marudio wa ubunge na udiwani wa
Januari 13, 2018 uahirishwe kwa kuwa mazingira ya uchaguzi hayako sawa.
Pia vimesema kama Serikali
na Tume ya Uchaguzi (Nec) itashindwa kutekeleza hilo, havitoshiriki katika uchaguzi huo.
Freeman Mbowe
Msimamo huo umetolewa leo
jijini Dar es Salaam na viongozi wa Ukawa walipokuwa wakizungumza na waandishi
wa habari.
Mwenyekiti wa Chadema taifa,
Freeman Mbowe amesema Nec ilipaswa ikae na wadau na vyama vya siasa kujadili
utaratibu mzima wa jinsi uchaguzi huo utakavyofanyika.
‘’Lakini tumeshtuka kuona
Nec inatangaza ratiba ya uchaguzi wa majimbo na kata pamoja na sheria
kuwaelekeza hivyo lakini kutoka na kutokuwepo kwa mazingira sawa na ukiukwaji
wa haki na sheria katika uchaguzi mdogo wa marudio wa udiwani,mazingira ya
kufanyika uchaguzi mwingine hayako sawa. Hivyo tunaiomba NEC na Serikali
kuahirisha uchaguzi huu na wakishindwa kufanya hivyo Ukawa hatutoshiriki
uchaguzi huo.’’ amesema Mbowe
Akitolea mfano amesema jimbo
la Longido Kaskazi halipo wazi na kuwa kuna rufaa imekatwa
katika mahakama ya rufani na wameijulisha tume lakini bado haijawajibu
Wametaka Nec ikae na wadau wake ikiwamo vyama vya
siasa kujadili suala hilo na kwamba uchaguzi si mapambano na ni lazima ufuate
taratibu, sheria na kanuni za uchaguzi .
‘’Kuna viashira vya kupoteza amani ya nchi, upo
ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu’’ amesema Mbowe
Kuhusu kwenda mahakama wanaamini kuwa wakati mwingine
inachelewesha haki ya msingi na kwamba
haki nyingine zinapatikana kwa kujadiliana nje ya mahakama.
Jimbo la Singida Kaskazini, Longido Kaskazini na Songea Mjini ndio majimbo yaliyotangazwa na Nec kurudia uchaguzi Januari 13, 2018
No comments:
Post a Comment