Makalla awapiga 'stop' wataalam kilimo kukaa ofisini...soma habari kamili na matukio360..#share
Mwandishi wetu Mbeya.
MKUU wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
amepiga marufuku wataalam wa kilimo kukaa ofisini na kwamba ni kinyume cha
sheria.
Pia amewaagiza wakurugenzi, wakuu
wa wilaya zote mkoani hapa  kuhakikisha
wanatenga hekta 100 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ikiwa ni utekelezaji  sera ya uchumi wa  viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika akimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Kikondo, Joba  Chriss  baada ya kukagua barabara yenye urefu wa kilometa zaidi ya 200   na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Sekta ya uwekezaji.
"Wataalam  wa kilimo ni marufuku kukaa ofisini, sasa ni
kuelekeza nguvu kwa wakulima. Kitendo
cha kutotekeleza majukumu yao ni kinyume cha sheria,"amesema.
Ametoa agizo hilo leo jijini Mbeya alipokuwa katika
mahojiano maalum na matukio360 na kwamba ni lazima maeneo yatengwe ili
kuhakikisha  serikali inafikia malengo ya
kutekeleza uchumi wa viwanda hususan kuwandaa wakulima kuzalisha mazoa yaliyo
na tija
"Sera ya viwanda
itafikiwa endapo wakulima watakuwa na afya njema na Serikali sasa inawekeza
zaidi katika sekta ya kilimo  hivyo ni
jukumu lenu wakurugenzi, wakuu wa wilaya kusimamia na kutenga maeneo kwa ajili ya
uwekezaji,"amesema Makalla.
Pia amewaagiza  kuweka kipaumbele  upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, wakulima
kupewa elimu ya kilimo kutoka kwa wataalam na si kuwaacha tu.
Makalla, pia amewataka  watendaji kuacha mara moja  tabia ya
kuwakaimisha maofisa ugani nafasi zao  jambo linalosababisha kushindwa kutekeleza
majukumu yao ipasavvyo.



No comments:
Post a Comment