Wakala serikali mtandao yataja mafanikio kumi....soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
WAKALA wa Serikali Mtandao kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi na
Utawala Bora, umeeleza mafanikio kumi ya utekelezaji wa serikali mtandao kwa
kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Serikali Mtandao Dk. Jabiri Bakari, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa
Wakala ya Serikali Mtandao Dk. Jabiri Bakari amesema “Ndani ya miaka mitano,
serikali imeijengea uwezo wa wakala ulioiwezesha kutekeleza jitihada a serikali
mtandao kwa kusaidia kusogeza huduma za taasisi za serikali karibu na umma,”.
Dk. Bakari ametaja mafanikio hayo kuwa ni kusimamia
utekelezaji wa viwango na miongozo ya serikali mtandao kwa taasisi za umma ili
kuwezesha utekelezaji wa serikali mtandao, zaidi ya hayo, wakala inatumia
viwango na miongozo hiyo kutoa maelekezo ya namna sahihi ya kutekeleza jitihada
za serikali mtandao na kupunguza urudufu.
Kuendesha vituo vya kuhifadhi mifumo na data zaa serikali
vinavyotoa huduma za kuhifadhi tovuti, mifumo tumizi, utunzaji katika sehemu
zaidi ya moja,“ co-locatio” na usajili na uhifadhi wa majina miliki.
Kutengeneza na kuendesha mtandao wa mawasiliano serikalini
(GovNet) ulio salama na nafuu ambao taasisi za umma 150 zikiwemo Wizara na Idara
za serikali, hospitali za mikoa na baadhi ya Ofisi za halmashauri.
Mengine ni kutoa huduma za ushauri kwa taasisi za umma 299 na
huduma za msaada wa kiufundi 2947 katika maeneo ya uhakiki wa mifumo ya Tehama,
tathmini ya usalama wa Tehama, utengenezaji wa mpango wa kukabili majenga,
utayarishaji wa mkakati wa Tehama, utayarishaji wa sera ya Tehama, na
utayarishaji wa usanifishaji wa shughuli na uhakiki wa miradi ya Tehama.
Kutoa mafunzo ya
kiufundi ya serikali matandao katika maeneo ya, usimamizi wa mtandao kwa
taasisi 240, mfumo wa baruapepe serikali kwa taasisi 359, utekelezaji wa huduma
mtandao kwa taasisi 76 na usimamizi wa tovuti kwa taasisi 411.
Kuhuisha na kusanifu upya tovuti ya serikali kuwa tovuti kuu
ambayo ni kituo kimoja cha kutolea taarifa na huduma mtandao kwa wananchi kwa
kupitia sehemu ya huduma za simu za mkononi na wavuti ya tovuti hiyo.
Kutengeneza na kuendesha mfumo wa huduma za serikali kwa
kutumia simu za mkononi (mGOV) kama kituo kimoja cha huduma zote za serikalini
kwa simu za mkononi ambapo jumla ya taasisi za umma 117 zinatumia mfumo huo na
zaidi ya miamala 15 milioni imefanywa.
Ameongeza, mfumo wa ofisi mtandao (GeOS) ulisanifiwa,
kutengenezwa na kutumika kuwezesha shughuli za kila siku za umma. Kwa sasa
taasisi n za umma 28 zimeunganishwa na kutumia mfumo huu.
Mfumo wa Serikali wa baruapepe (GMS) ulisanifiwa,
kutengenezwa na kutumika, kuwezesha mawasiliano ya ofisi ambapo jumla ya
taasisi za umma 359 zikiwemo ofisi za
ubalozi zimeunganishwa na zinatumia mfumo huu.
Na Wamewezesha usanifu na utekelezaji wa mifumo mbalimbali
inayowezesha utendaji kazi katika taasisi za umma ikiwemo mfumo wa kutoa
taarifa za rushwa (Takukuru kupitia namba 113), mfumo wa taarifa na shughuli za
bunge, mfumo wa ajira unaorahisisha mchakato wa ajira za serikalini na mfumo wa
malipo ya serikali kielekroni (GePG) unaowezesha udhibiti wa ukusanyaji wa
maduhuli kielekroni serikalini.
Amesema wamejizatiti vyema kuanza kipindi kingine cha miaka
mitano ya utekelezaji kuanzia 2016/2017 hadi 2020/2021 ili kufanya matumizi ya Tehama yawe na manufaa
zaidi katika utendaji wa taasisi za
umma.




No comments:
Post a Comment