Makamba: Viongozi muwe na maarifa.....soma habari kamili na matukio360..#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira,
January Makamba amewashauri viongozi nchini kuwa na maarifa na kwamba uongozi si cheo bali ni mamlaka.
Waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa rais, muungano na mazingira, January Makamba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo
ya siku mbili ya uongozi na maadili kwa wanafunzi viongozi wa vyuo vya elimu ya
juu nchini yaliyoandaliwa na Shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu (TAHLISO),
ili kuwajengea uwezo wa uongozi.
Amesema kiongozi si cheo bali ni mamlaka kwani unaweza kuwa na
cheo na usiwe na mamlaka kwa unaowaongoza.
"Unakuwa na cheo lakini kuna kufuatwa na kutiiwa na ili uwe
na manufaa kwa watu lazima uweze na uwe na maarifa ya kusaidia watu na
kuwashirikisha katika mambo yanayowahusu," amesema.
Amesema kiongozi anapaswa kuishi kwa mfano na tabia njema na si
uwezo wa kusherehesha watu jukwaani.
Amesema lazima nchi iwe na utaratibu wa kuandaa na kuwajengea
uwezo na maarifa viongozi katika vyuo vyao huku akibainisha mambo yasiyitakiwa
kama ulevi, usinzi, dawa za kulevya, uasherati, chuki, ukabila hapaswi kuwa
navyo.
"Tunafarijika katika mafunzo haya kuna mada mbalimbali
ikiwemo maadili ya uongozi, kupambana na dawa za kulevya,miiko ya rushwa,
kujitambua na mazingira ya uongozi.
"Vijana hawa wakijengwa kwenye maadili, taifa litapata
viongozi wazuri, "amesema.
Kwa upande wake, Katibu Sekretarieti ya maadili, Idara ya
Viongozi wa siasa, Waziri Kipacha amesema wameanzisha klabu za maadili
kuanzia ngazi ya shule za msingi hadi vyuo.
"Mafunzo haya ni sehemu ya jukumu la sekretarieti ya
maadili katika kukuza na kujenga uadilifu kwa vijana ngazi za
shule,"amesema.
Amesema mafunzo hayo yatawaandaa wanafunzi hao kujua maadili
ambayo kiongozi wa umma anapaswa kuwa nayo pindi anapoteuliwa
No comments:
Post a Comment