Maombi ya CUF Lipumba kumkataa jaji yatupwa...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Dar es
Salaam
MAHAKAMA kuu jijini Dar es Salaa
leo imetupilia mbali maombi ya kumtaka Jaji Wilfred Ndyansobera ajitoe
kusikiliza mashauri ya CUF yanayoendelea katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam
Profesa Ibrahim Lipumba
Maombi hayo yaliwasilishwa
mahakamani hapo na watu 10 wanaodaiwa kuwa ni wajumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF
ya Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa
Ibrahim Lipumba, ambapo barua ya maombi hayo ilikuwa na malalamiko sita ikiwemo
wadaiwa kutokuwa na imani na jaji.
Akisoma maamuzi ya kutokujitoa
kusikiliza mashauri hayo leo mbele ya mahakama, Jaji
Ndyansobera, amedai kuwa baada ya kuchunguza malalamiko hayo, na kusikiliza
hoja za mawakili wa pande zote mbili, amegundua kuwa hakuna kitu kinachoonyesha
kama anapendelea upande mmoja, pia malalamiko hayo yalikuwa si sahihi kisheria
kutokana kwamba watu 10 waliowasilisha maombi hayo, ni watu binafsi na si bodi
halali ya wadhamini ya CUF.
“Bodi ya CUF ina taratibu
zake za kutekeleza majukumu yake, mtu hawezi kusema anatumwa na bodi, bali bodi
hufanya kazi zake. Jaji kujiondoa sio kitu chepesi ni kitu kizito,” amesema.
Jaji Ndyansobera amedai
kuwa, katika kusikiliza mashauri ya CUF, alifuata sheria na katiba ya nchi,
ambapo sheria inamtaka jaji kutekeleza majukumu yake katika kutoa haki, bila ya
woga wala upendeleo au shinikizo kutoka upande wowote.
“Kuna mambo mawili ya msingi
ya kuzingatia, jaji anatakiwa kujiondoa kwa kuzingatia mazingira ya kesi kama
alikuwa anapendelea… pili kama kuna uhusiano wa karibu na mtu mmojawapo kwenye
kesi au masilahi binafsi, jaji inatakiwa ujiondoe. Mahakama inatakiwa kuwa
huru, jaji au Mahakama inaweza kuamua kesi kwa kuzingatia ushahidi ulioko mbele
yake pasipo kupata mashinikizo kutoka nje na ubaguzi,” amesema.
Hali kadhalika ametaja
sababu tano zilizopelekea kutokujitoa katika kusikiliza mashauri hayo, ikiwemo
kuzuia ucheleweshwaji wa kesi, upotevu wa fedha, pia Jaji aliyekuwepo
(Ndyansobera) ameshatoa maamuzi kwenye baadhi ya kesi hivyo inabidi aendelee
kusikiliza mashauri kutokana kwamba anazijua kesi vizuri.
No comments:
Post a Comment