Mabunge EAC yatakiwa kuongeza bajeti katika michezo ...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Suleiman Msuya
MABUNGE ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yametakiwa
kutenga bajeti za michezo za kutosha ili kuongeza ufanisi wa mashindano ya
mabunge hayo yanayofanyika kila mwaka.
Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ya kuzitaka nchi hizo imetolewa na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harrison Mwakiyembe wakati akifunga mashindano
ya nane ya michezo ya mabunge hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema amepata taarifa kuhusu bajeti hivyo ni matumaini yake
kuwa katika mashindano yajayo changamoto hiyo haitakuwepo.
Dk.Mwakiyembe amesema ni jukumu la mabunge kutenga bajeti nzuri
kwa ajili ya michezo ili kuhakikisha kuwa yanashiriki bila hofu yoyote katika
mashindano mbalimbali.
Waziri amesema iwapo mabunge yatatenga bajeti inayotosheleza ni
dhahiri kuwa ushindani utakuwepo wakati wa mashindano .
"Hamjasema katika risala yenu kuhusu ufinyu wa bajeti
lakini najya bajeti zenu ni ndogo sana nadhani wakati umefika kwa kuwepo bajeti
ya kutosha ya michezo ili kuleta ufanisi," amesema.
Ametoa rai kwa bunge kutumia wizara ya michezo ili kuweza
kuweka mazingira rafiki ya kuhakikisha ushiriki mkubwa wa wananchi katika
mashindano hayo kwa miaka ijayo.
Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk Ackson Tulia amesema mashindano hayo yanapaswa kutumika kudumisha mshikamano, umoja na
ushirikiano baina ya nchi zao na wananchi.
Dk.Ackson amesema katika mashindano hayo ya nane ambayo
yalishirikisha zaidi ya wabunge na watumishi 800 kutoka nchi za Burundi,
Uganda, Kenya, Bunge la Afrika Mashariki (EALA) na Tanzania yalifana pamoja na
changamoto kidogo zilizotokea.
Amesema mashindano hayo yanapaswa kuwa endelevu kwani yamekuwa
na mchango mkubwa katika kukuza umoja, ushirikiano na mshikamano kati ya nchi
wanachama.
"Mashindano haya yalianza Desemba mosi na yamemalizika jana
kwa mafanikio makubwa sana naamini mashindano ya mwakani ambayo yatafanyika
nchini Uganda yataboreshwa zaidi," amesema.
Naibu Spika alisema ni imani yake kuwa mashindano yajayo
yatarekebisha kasoro ambazo zimejitokeza hasa katika mchezo wa pete ambapo
kulikuwa na mgogoro kidogo.
Amesema katika mashindano hayo michezo saba ilichezwa ambayo ni
gofu, riadha, pete, wavu, mpira wa miguu, kuvuta kamba na kutembea kwa kasi.
Dk.Ackson alisema Bunge la Tanzania limefanikiwa kuibuka na
vikombe vitatu ambavyo ni vya kuvuta kamba, kutembea kwa kasi na mbio za
kupokezana vijiti wanawake.
"Uganda wamepata vikombe katika mpira wa miguu, wavu
wanawake na gofu huku Kenya wakibuka videdea katika riadha wanaume na wanawake,
wavu wanaume na Burundi wakipata tuzo ya timu bora," alisema.
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, William Ngeleja alishukuru
Bunge la Tanzania kufanikisha mashindano hayo kwa ufanisi na usalama wa kutosha
na kwamba sasa wanajiandaa na mashindano ya mwakani.
Ngeleja amesema ni matarajio yake kuwa changamoto zilizojitokeza
zitafayiwa kazi kwenye mashindano mengine ya mwakani.
No comments:
Post a Comment