Mbunge Lijualikali, Suzan Kiwanga mambo magumu....soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu
MBUNGE Peter Lijualikali wa
Kilombero na Suzan Kiwanga wa Mlimba wote
kwa tiketi ya Chadema na wenzao 37 wamerejeshwa rumande kufuatia hakimu wa kesi
hiyo, Ivan Msack kuwa mgonjwa.
Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga
Wabunge hao na wenzao leo
wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro ambapo mahakama ilitakiwa
kutoa uamuzi wa dhamana lakini imeshindikana hadi Desemba 8, 2017.
Hakimu wa mahakama hiyo
Erick Rwehumbiza amesema hakimu Ivan amepata maradhi ya ghafla na yupo katika
matibabu.
Upande wa utetezi ukiongozwa
na wakili Peter Kibatala umesema kuhahirishwa kwa kesi hiyo na kutotolewa
dhamana kwa washtakiwa kunalenga kuchelewesha upatikanaji wa haki.
Awali Kibatala alitaka keshi hiyo iamishwe kwa
hakimi mwingine lakini hoja yake hiyo ilipingwa na hakimu Rwehumbiza.
Jana Kulitokea mvutano kati
ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kuhusu hati ya kiapo ya kupinga dhamana
iliyowasilishwa mahakamani hapo.
Kutokana na mvutano wa kisheria,
hakimu Ivan Msack aliahirisha kesi hiyo hadi leo Jumatano Desemba 6,2017 ili
kutoa fursa kwa pande zote mbili kujibu hoja kuhusu hati hiyo.
Washtakiwa wanakabiliwa na
mashtaka nane likiwamo la kuchoma moto ofisi ya Kata ya Sofi iliyopo wilayani
Malinyi.
Washtakiwa wanatetewa na
mawakili Peter Kibatala, Ignas Punge, Fredrick Kiwelo na Bartholomew Tarimo.
Upande wa mashtaka
unawakilishwa na mawakili wa Serikali, Edga Bantulaki na Sunday Hyera.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa
kamati kuu ya chama hicho, Frederick Sumaye walihudhuria mahakamani.
Wengine waliofika mahakamani
ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na wa Viti Maalumu, Devota Minja.
No comments:
Post a Comment