Waziri Mwijage: Msikamate ovyo bidhaa za watanzania..soma habari kamili na matukio360..#share
Na Salha Mohamed
WAZIRI wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage
amezitaka mamlaka za serikali kuelewesha watu kujua viwango vya bidhaa
wanazopaswa kuzalisha na si kuwakamata kwa kutojua viwango.
Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage akifungua warsha ya wadau wa kilimo leo jijini Dar es Salaam
Mwijage ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam
alipokuwa akifungua warsha ya kitaifa siku mbili ya wadau wa Kilimo iliyoandaliwa
na Baraza la Kilimo Tanzania (ACT).
"Ili twende vizuri na kufanikiwa katika sekta ya
viwanda. Mamlaka zote za serikali
zisifanye kazi ya upolisi zifanye kazi ya ualimu nalisema hilo na nipo tayari
kuhukumiwa, "amesema.
"Mtu anafanya 'packaging' anatengeneza bidhaa
yake mnamwambia amekosea umweleze maana yake ni nini.... Muwafundishe hao watu
ambao mimi napoteza muda kuwahamasisha kujenga viwanda, "amesema na
kuongeza. "Mimi siwezi kushawishi
halafu mwenzangu anafungia. Kwa sasa mazingira ya biashara ni
mazuri."
Amesema serikali itaendelea
kuimarisha mazingira ya kufanya biashara na kuwa mtu anayetaka kuweka kiwanda aanze halafu
mamlaka ya mazingira na mamlaka ya viwango (TBS) wafuate.
"Tunajenga viwanda ili
tutengeneze soko la mazao yenu, viwanda ni masoko tunajenga viwanda kwasababu asilimia 65 ya watanzania
ni vijana na wengi Hawana kazi, "amesema.
Waziri Mwijage amesema
ujenzi wa viwanda si kuzalisha bidhaa pekee bali ni pamoja na kutengeneza
ajira.
Awali, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa ACT, Dk.
Sinare Sinare amemshukuru rais kwa kuwaondolea tozo katika mazao.
Amesema wanaamini kichocheo cha uzalishaji ni soko na
changamoto iliyopo ni soko kwa nchi za
Afrika Mashariki.
"Afrika Mashariki hakuna mchele unaopendwa kama
unaotoka Tanzania, lakini fursa hiyo inashindwa kutumika ipasavyo kutokana na mwingiliano wa masoko, "amesema.
Amemwomba waziri, kutenga asilimia 10 ya bajeti ya
serikali kuwekeza kwenye kilimo ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya
kilimo.




No comments:
Post a Comment