Mtanzania afariki ndani ya ndege akiwa amebeba dawa za kulevya...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu
MTU mmoja anayedaiwa kuwa ni mtanzania amekutwa amefariki
ndani ya ndege akiwa amebeba dawa za kulevya tumboni.
Kamishna wa kupambana na dawa za kulevya, Rogers William Sianga
Umauti huo umemkuta ndani ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia na kwamba alikuwa akielekea
nchini China.
Kamishna wa kupambana na dawa za kulevya, Rogers William
Sianga amethibitisha taarifa hizo na kwamba uchunguzi unaendelea kuhusu tukio
hilo.
"Ni kweli hata sisi tumepokea taarifa za kifo hicho cha
Mtanzania ndani ya ndege ya Ethiopia. Tunaendelea na mchakato wa kiuchunguzi,’’
amesema Sianga
Imeelezwa hivi sasa kumekuwapo na ongezeko la watanzania wanaotumika
kusafirisha dawa za kulevya kwenda nje ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment