Mwijage: Tutawawezesha wajasiliamali....soma habari kamili na matukio360..#share



Na Salha Mohamed,Dar es salaam

SERIKALI imesema haitashusha viwango vya ubora wa bidhaa kwa wajasiliamali wadogo na kwamba  itawawezesha ili kuendana na matakwa ya soko.  
Charles Mwijage

Waziri  wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi ya Tanzania Growth Trust(TGT) inayowawezesha wajasiliamali wadogo. 

Waziri Mwijage amesema aamini katika changamoto za wajasiliamali,kinachohitajika  ni elimu. 

"Elimu ikipatikana yote yatakuwa sawa... Wanamatatizo na Shirika la viwango lakini sisi hatutapunguza viwango kama ni chakula, vinywaji viwango hatutavipunguza ila tutamuwezesha mjasiliamali wa kitanzania aweze kufikia viwango hivyo, "amesema. 

Amesema kwa kufanya hivyo kutawawezesha wajasiliamali hao kutoa bidhaa zenye viwango katika soko na kupata uimara wa ushindani kwenye soko la kimataifa. 

Amesema wapo wajasiliamali ambao huuza bidhaa zao nje ya nchi  huku akiwaasa wajasiliamali kutosheleza soko la ndani.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TGT, Olive Lwena amesema wajasiliamali hawajiamini na kutaka kubaki walipo. 

"Hata waziri amesema wajasiliamali wengi wanamatatizo na TFDA na TBS, waziri kawaita wahusika na watalitatua lakini kuna changamoto ya mitaji, "amesema. 

Amewaasa vijana kutafuta fursa katika mashirika na si kukata tamaa au kutaka hela kwa muda mfupi bila kuwa mbunifu ,uvumilivu na kujituma ili wayaone matunda.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search