Meya Mwita huyo Marekani...soma habari kamili na matukio360..#share

Na Christina Mwagala

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita leo ameondoka  kuelekea Chicago nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa mameya duniani utakaofanyika Desemba 4 hadi 7, 2017.


Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita

Mkutano huo unatarajiwa kuhusisha mameya 182 kutoka sehemu mbalimbali Dunia pamoja na mambo mengine watajadili suala la utawala bora  na utumishi wa viongozi kwa wananchi.

Pia wataangalia na kujadili changamoto za majiji makubwa hususani katika sekta ya afya, miundombinu, maji safi na salama, elimu  na mabadiliko ya tabia  nchi.

Desemba  5, mameya wote waliohudhuria mkutano huo kwa pamoja watashindanisha majiji yaliyofanya vizuri katika sekta ya miundombinu. Jiji la Dar es Salaam limeingia kwenye ushindani huo kupitia  mradi wa mabasi yaendayo haraka.

Katika ushindani huo, Meya Mwita amesema  ana amini jiji la Dar es Salaam litaibuka mshindi wa tuzo hiyo kwa kuwa mradi huo umekuwa ukifanya vizuri katika sekta ya  usafirishaji na  watanzania wajiandae  kupokea tuzo hiyo.

Majiji mengine ambayo yanameingia kwenye ushindani huo ni mji wa Cape Town na Cairo . Meya  huyo atarajea nchini Desemba 8, 2017.




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search