Serikali yahimiza uwepo vituo vya ukaguzi wa miozi mipakani...soma habari kamili na matukio360..#share


Na mwandishi wetu
NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha ameiagiza Tume ya Nguvu za Atomiki kuhakikisha inaweka vituo vya ukaguzi wa viwango vya mionzi kwa bidhaa zote zinazoingia na kutoka nchini katika mipaka yote kwa lengo la kudhibiti mionzi katika bidhaa hizo.



Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha  kushoto akitoa   maelezo kwa wataalam  wa  Tume ya Nguvu za Atomiki

Ametoa agizo hilo leo  jijini Arusha alipotembelea Tume hiyo ili kujionea jinsi inavyofanya kazi,  amesema ni muhimu vituo hivyo kuwekwa katika mipaka  ili  kuhakikisha bidhaa zinazoingia na kutoka nchini zinakuwa na viwango vya mionzi inayokubalika kimataifa.

Pia ameitaka Tume hiyo kutoishia katika kutekeleza majukumu ya kudhibiti na kuhamasisha matumizi bora ya mionzi bali inapaswa kuanza kuangalia namna bora ya kuhamasisha matumizi chanya ya nyuklia kwa maendeleo ya taifa katika nyanja za afya,  kilimo,  maji  na teknolojia.

Naibu Waziri Nasha pia  ametembelea na kukagua  maendeleo ya ujenzi wa maabara ya kisasa kwa ajili ya upimaji wa ubora wa vifaa mbalimbali vya mionzi ikiwemo vifaa tiba vya Tume hiyo, maabara hiyo inajengwa na fedha za serikali kiasi cha shilingi bilioni mbili.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa tume ya nguvu za Atomiki, Brigadia Jenerali Fulgence Msafiri amesema kutokana na upungufu mkubwa wa watumishi walio na weledi katika teknolojia ya nyuklia imefanya taasisi  hiyo kukosa  watumishi kutokana na kuanzishwa kwa vituo vya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa katika mipaka ya Rusumo,  Mtukula,  Kabanga, Kigoma,  Tunduma,  Kasumulu na Daraja la Mkapa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search