Mzee miaka 73 aeleza yanayomkuta baada ya kuachiwa huru ....soma habari kamili na matukio
MZEE wa miaka 73 Issa Mwema Issa ambae alidaiwa kutorosha msichana wa miaka 12 na kuhukumiwa kifungo cha miaka nane na kuachiwa huru amesema kuwa amekuwa katika wakati mgumu kutokana na kukosa ushirikiano kwa jamii tangu atoke jela.
Mwema ambae alitumikia kifungo hicho kwa muda wa miezi mitatu na kuachiwa huru na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Makungu ambae alidai kuwa ushahidi wa kesi hiyo ulikuwa ni wa kupangwa.
Mzee Issa Mwema
Alisema kuwa pamoja na kuwa yupo huru lakini hana faraja kutoka kwa wanajamii wa hapo ikiwemo pia kukimbiwa na aliekuwa mke wake wa ndoa ambae alidai talaka na kumuacha.
“Nashukuru nimetoka jela lakini sina maisha ya furaha kwa jamii kwani imenitenga na sina ushirikiano wowote, hili limeniathiri, pia nimekosa mke”, alisema.
Alisema kuwa kabla hajafikwa na mkasa huo alikuwa ni mtu mashuhuri katika kijiji hicho kwa kushirikishwa katika shughuli zote za kijamii ikiwemo kusalisha na kuosha maiti lakini kwa sasa hashirikishwi kwa lolote
Hata hivyo alisema kuwa baada ya kuona hivyo ameamuwa kupumzika na kuacha shughuli hizo zifanywe na watu wengine.
“Nimeamua niachane nayo kwani nimekuwa nikijiuliza wakati mimi sipo shughuli hizo zilikuwa hazifanyiki”, alisema Mzee Issa.
Alisema kuwa kuachiwa kwake huru hakumainishi kwamba alikuwa na uhusiano na jaji huyo na wala hakumshirikisha mtu yoyote katika kesi yake hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa baada ya kupata matatizo hayo sasa hivi amekuwa na woga mkubwa hata kumsaidia mtoto ambae atakuwa na tatizo kwa kuhofia kuwa amemfanyia udhalilishaji wa kijinsia.
“Mie nasema kuwa kwa sheria za ubakaji zilivyo kwa sasa hata ukimuona mtoto analia pale utaogopa kumsaidia au kumuuliza kwa kuhofia kuambiwa umembaka," alisema.
Hata hivyo Mwema aliongeza kwa kusema “na haya tujiepushe nayo kuwapa pesawatoto kwa sababu akienda kwao ulikuwa ukilia umefanya nini hata kapigwa na mtoto mwenziwe lakini akionekana na pesa umempa wewe utaambiwa umembaka”.
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu ambae alifanya mapitio jalada la kesi hiya ambayo ilihukumiwa katika mahakama ya wilaya Makunduchi alisema kuwa aliigunduwa kuwa ushahidi ni wa kupangwa na hakimu ambae aliihukumu kesi hiyo alitoa hukumu kwa presha za wanaharakati.
@@@@@@@@@@@2
caption
Issa Mwema Issa mzee alidaiwa kutorosha na kuachiwa huru na jaji mkuu wa Zanzibar kwa madai ushahidi wa kesi yake ni wa kupangwa akizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini kwake Makunduchi kuzungumzia hali halisi ya kuachiwa kwake huru pamoja na kadhiya anayoipata
kutoka kwa jamii.
caption
Issa Mwema Issa mzee alidaiwa kutorosha na kuachiwa huru na jaji mkuu wa Zanzibar kwa madai ushahidi wa kesi yake ni wa kupangwa akizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini kwake Makunduchi kuzungumzia hali halisi ya kuachiwa kwake huru pamoja na kadhiya anayoipata
kutoka kwa jamii.




No comments:
Post a Comment