Naibu waziri akemea vitendo vya ushoga shule za dini...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Alex Stephen
SERIKALI imesema shule za taasisi za dini zimepoteza
mwelekeo kwa kuanza kuzalisha vijana wa vijiweni na baadhi kujiingiza katika
vitendo vya ushoga.
Naibu katibu mkuu wizara ya elimu, Dk Ave Maria Semakaf
Kauli hiyo imetolewa leo na naibu katibu mkuu wizara ya
elimu, Dk Ave Maria Semakaf wakati akifungua mkutano wa umoja wa shule za
seminali na binafsi uliofanyika mjini Dodoma.
Semakafu alikemea tabia ya ushoga kuwa imeanza kuota
mizizi kwani vijana wengi wa mitaani wakiulizwa mambo ya ushoga walijifunzia
wapi wanazitaja shule za dini.
"Haya siyo maadili mliyokuwa mkifundisha tangu
awali, kafundishe maadili ya kidini kama mlivyokuwa awali, tunapata malalamiko
mengi kutoka kwa wazazi na wanafunzi wanaosoma huko kuhusu tabia hizo
chafu,"amesema Semakaf




No comments:
Post a Comment