Mkurugenzi Nkasi asimamishwa kazi, atuhumiwa kuchota bilioni 7...soma habari kamili na matukio360..#share

Alex Stephen
WAZIRI wa nchi ofisi ya rais Tamisemi, Seleman Jafo amemsimamisha kazi mkurugenzi wa wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Julius Kawondo kwa tuhuma za rushwa na  matumizi mabaya yaliyoisababishia serikali hasara ya bilioni  7


Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo

Leo mjini Dodoma Jafo amewaambia waandishi wa habari kuwa Kawondo ameshindwa kusimamia kile alichopaswa kukifanya kwa wakati katika eneo lake la utumishi.

"Natumia sheria ya serikali za mitaa sura ya 4 kifungu cha kwanza hadi tano pamoja na sura ya 287 ya sheria hiyo ambavyo vinanipa mamlaka hayo," amesema Jafo

Amesema fedha hizo zilikuwa za mradi wa maji wa kijiji cha Kamwanda ambako mkurugenzi alishirikiana na mmoja wa maofisa kutoka wizara ya maji.

Hivyo amemuomba waziri wa maji na umwagiliaji, Isaak Kamwelwe kumchunguza mmoja wa watumishi katika wizara yake ambaye alishirikiana na mkurugenzi huyo kuhujumu mradi wa maji katika kijiji cha Kamwanda wilayani humo.

Katika mkutano wa nane wa bunge, mbunge wa Nkasi Kaskazini Ali Keissy alilalamika bungeni akimtaka rais akamkabidhi watumishi wake kwani ni wabadhirifu.

Keissy alisema miradi ya maji ndiyo inaonekana kuhujumiwa zaidi ikiwemo kununua vitu bandia na kufanya udanganyifu kwenye manunuzi


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search