'Nchi yangu kwanza' kuzinduliwa Desemba 8...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
KAMPENI ya kitaifa ya
uzalendo na utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ inatarajiwa kuzinduliwa kupitia ‘usiku
wa kitendawili’ Desemba 8, 2017 mjini Dodoma.
Rais John Magufuli (kushoto) na Mrisho Mpoto (kulia)
Usiku wa Kitendawili
ulianzishwa baada ya msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kuachia
wimbo ‘Kitendawili’ na baadaye kufikiria kuanzisha usiku wa wimbo huo na
kuanzisha mjadala kuhusu uzalendo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Msanii wa muziki
wa asili nchini, Mrisho Mpoto kupitia Kikundi cha Sanaa cha Mpoto Theatre
Gallery na wadau wa sanaa za Ubunifu ambao ndio waratibu usiku huo na Wizara ya
Habari Sanaa utamaduni na Michezo, amesema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais
John Magufuli.
“Usiku wa kitendawili
utatumika kama jukwaa la kuwaleta pamoja watanzania pamoja na viongozi wao ili
kukumbushana kuhusu wajibu na kujadili mustakabali wa Taifa. Kutakuwa na
vivutio mbalimbali pamoja na wimbo maalumu kutoka kwa wasanii maalumu Mwaka
Huu,” amesema Mpoto.
Amesema lengo la kampeni
hiyo ni kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zinazojitokeza
nchini na itakuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha
Baba wa Taifa, Hayati Julis Kambarage Nyerere.
Amebainisha kwamba mambo
ambayo yatafanyiwa kazi katika kampeni ni kudhibiti na kukomesha mmomonyoko wa
maadili kwa viongozi wa Umma, rushwa, ufisadi, ubadhilifu wa mali za Umma na
kuongeza hari ya kufanya kazi na Uzalendo.
Amesema baada ya uzinduzi
huo mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma,
itafanyika kwenye mikoa yote nchini na itasimamiwa na Kamati za Utamaduni chini
ya wenyeviti wakuu wa mikoa na wilaya.
No comments:
Post a Comment