Nicol waomba Takukuru kuchunguza hasara bilioni 9...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu
WANAHISA wa kampuni ya uwekezaji
ya Nicol, wameazimia uongozi uliopita, ukiongozwa na Felix Mosha ulipe gharama
za kesi 41 walizozifungua katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa kama
ilivyoamuriwa na mahakama hizo ama mali zao zifilisiwe.
Pia wameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuingilia kati na kuchunguza hasara ya bilioni 9.4 iliyopatikana mwaka 2009.
Mwenyekiti wa kampuni ya Uwekezaji wa Taifa (NICOL) Dk Gideon Kaunda kulia na kushoto ni Mtendaji Mkuu Adam Wamunza.
Maazimio hayo yamefikiwa
Desemba 2, 2017 katika mkutano mkuu wa tatu wa mwaka wa wanahisa wa Nicol ,
ulifanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
‘’ Pia tunataka wahusika
wote waliofungua kesi katika mahakama mbalimbali waondoe kesi hizo ndani ya mwezi mmoja na ikishindikana menejimenti ichukue hatua.’’
Mwenyekiti wa bodi ya Nicol,
Dk Gideon Kaunda alieleza kuwa uongozi uliokuwa ukiongozwa na Mosha
ulisababisha hasara kufikia mwaka 2009
ya Sh 9.4 bilioni.
A,esema Mosha aliiruka bodi yake na kufanya
alivyotaka, kuupuza maagizo na miongozo mbalimbali iliyotolewa na mamlaka za
udhibiti kwa kutumia vibaya nafasi yake
kama Mwenyekiti wa Nicol ikiwa ni pamoja na utekelezaji mbaya wa taratibu za
bodi.
Aliongeza kuwa mamlaka ya
masoko na mitaji ilimsimamisha kazi Mosha na bodi aliyokuwa anaiongoza lakini
ilipuuza amri ya kusimamishwa na kwamba
kutokana na ujeuri huo na kwa madhumuni ya kuinusuru kampuni wanahisa waliomba na kupata ruhusa ya mahakama kuutwaa uongozi wa Nicol kwa madhumuni ya kiunda upya kwa kumteua,
Interim Maneja na kumpa jukumu la
kuitisha mkutano wa dharura wa wanahisa.
“Mkutano huo uliitishwa
Aprili 14,2012 wanahisa waliivunja bodi iliyokuwa inaongozwa na Mosha na kuteua
bodi nyingine ambayo ilipewa jukumu la kukagua uwekezaji uliokuwa umefanywa ,
kutathmini ‘viability ya Nicol’ na
kuitisha mkutano mkuu wa wanahisa,’’ amesema Dk Kaunda.
Aliongeza kuwa Mosha aligoma kutambua na kukubali maamuzi
yaliyofanywa na wanahisa na akafungua moja kwa moja au kupitia mawakala kesi
zaidi ya 41 katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa, kesi zote zililenga
kumrudisha madarakani na kwamba aweze kudhibiti akaunti za Benki za Nicol.
Hata hivyo amesema Mosha
hakuwahi kupata ushindi katika kesi zote hizo na kwamba uwepo wa kesi hizo
uliathiri bodi mpya katika utekelezaji
wa majukumu iliyopewa na wanahisa.
Ilibainishwa kuwa pamoja na
vikwazo hivyo, bodi mpya ilifanikiwa kuweka kumbukumbu sawa za wakurugenzi wa
Nicol katika rejesta ya makampuni Brela, ilifanikiwa kulipa madeni yalikuwa
yamefichwa na Mosha ikiwa ni kumlipa
mwanahisa chini ya makubaliano yaliyofikiwa katika kesi ya madai namba 24,2013 dola za Marekani 2 milioni,
zikiwa ni albaki ya dola milioni sita alizoipatia Nicol kufanikisha ununuzi wa
hisa za National Microfinance Bank.
Kulipa Sh 402,234,678.79
ikiwa ni malimbikizo ya kodi ya
pango ya ofisi zilizotumiwa na Nicol kwa
miezi 37 pamoja na kulipa deni la kodi za serikali la Sh 556,785,241 na michango ya
wafanyakazi kwa akiba za uzeeni
yaliyofikia Sh 249,514,422.
Dk Kaunda, hata hivyo naye aliunga mkono uongozi
uliokuwa ukiongozwa na Mosha walipe gharama hizo za kesi ambazo mahakama
iliamuru walipe ama Mali zao zifilisiwe.
Jaji Mark Boman naye
alipendekeza walipe gharama zote za kesi
na iwapo itashindikana Mali zao zifilisiwe.
Mwanahisa, Emmanuel David
kutoka Arusha yeye aliomba wafilisiwe na wafikishwe mahakamani.
Mwanahisa Halidi Ramadhani
yeye aliomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iingilie kati kuchunguza suala la upangaji wa
ofisi ya Nicol katika Jengo la Raha Tower kama fedha hizo ni kweli zilipelekwa
kwa wahusika ama mifukoni.
David Robi mwanahisa kutoka
Mwanza yeye aliomba Mali zao zitambuliwe kwa kuwa mtoto akililia wembe ni
lazima umkate kwa nini tunawahurumia na kwamba fedha zinazoendelea kulipwa
zisitishwe.
Ilidaiwa kuwa pamoja ya kuwa
hakuwahi kupata ushindi kwenye kesi hizo , uwepo wa kesi hizo uliathili bodi
mpya katika utekelezaji wa majukumu iliyopewa na wanahisa.
No comments:
Post a Comment