Polepole: Wabunge CUF, Chadema Dar es Salaam kujiunga CCM...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu
CHAMA cha Mapinduzi(CCM) kimedai kuwa baadhi ya wabunge
wa Chadema na CUF wa majimbo ya Dar es Salaam wanataka kujiunga na chama hicho.
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole
CCM inatoa kauli hiyo wakati kukiwa na minon’gono kuwa
viongozi waandamizi wa upinzani wanaojiunga CCM wananuliwa huku chama hicho kikikanusha
na kutoa sababu kuu mbili ya kupata
wanachama hao.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na
matukio360 jijini Dar es Salaam wiki
iliyopita katika ofisi ndogo za makao
makuu ya CCM, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema baadhi
ya wabunge hao wameonesha nia ya kujiunga na chama hicho.
Bila kutaja idadi wala majina ya wabunge hao Polepole amesema
“Wewe utaona ‘soon’ muda si mrefu kuna wabunge kutoka majimbo ya Dar es Salaam
wa UKAWA wameonesha nia ya kutaka kujiunga CCM.’’
Kuhusu sababu za wapinzani kujiunga CCM Polepole amesema
ni uongozi na utendaji mbovu wa viongozi wa kitaifa wa vyama vya upinzani ambao
hauzingatii kanuni na taratibu zao
“Ukweli hawa viongozi waandamizi wa upinzani
wanaojiunga CCM hatuwarubuni wala kuwapa fedha. Watu hawaelewi wala kufuatilia
kwa undani, wengi wa waliojiunga CCM ukizungumza nao wanakueleza kuwa wamechoka
na jinsi wanavyoongozwa na viongozi wao wa kitaifa,’’ amesema na kuongeza
“Wanasema wanaweza kufanya maamuzi fulani ndani ya
chama na kwa kufuata utaratibu halali ikiwemo kuchaguana lakini mwenyekiti taifa anakuja na kutengua maamuzi hayo ‘so’ hivyo
unatarajia nini kitatokea hapo. Lazima sintofahamu itajitokeza.’’
Polepole ametaja sababu nyingine ni kukubali utendaji wa rais Magufuli hasa
anavyoshughulikia masuala ya ufisadi na rushwa.
“Hili la kupambana na ufisadi na rushwa wao wenyewe
wanalizungumza hivyo ni mojawapo ya mambo yanayowavutia kujiunga CCM,’’ amesema
Hata hivyo kufuatia utete wa hali hiyo hii leo ofisi ya mbunge wa Temeke imekanusha vikali
uvumi wa mbunge wa jimbo hilo, Abdallah Mtolea(CUF) kujiuzulu ubunge.
Katibu wa mbunge huyo, Rajab Matata amesema “Ukweli ni
kwamba aliejiuzulu ubunge ni Mh. Maulid Said Abdallah Mtulia aliekuwa Mbunge Wa
jimbo la Kinondoni. Na sio Abdallah Ali Mtolea Mbunge wa jimbo la Temeke.
Mtolea hajajiuzulu na hana mpango Wa kujiuzuru, anawaudumia wakazi wake wa Temeke.”
Amesema wanaomuhusisha na upotoshaji huo ni watu wasio
na nia njema na wenye lengo la kuwasumbua wananchi wa Temeke na watanzania.
Jana aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kinondoni(CUF)
Maulid Mtulia alijiuzulu wadhifa wake huo na kujivua uanachama wa CUF pamoja na
nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho na Bungeni.
Mtulia anakuwa ni mbunge wa pili katika kipindi cha takribani
mwezi mmoja kujiuzulu nyadhifa hiyo
baada ya aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii katika serikali ya awamu ya nne, Lazaro Nyalandu
kung’atuka CCM na kujiuzulu ubunge wa Singinda Kaskazini
No comments:
Post a Comment