Nicol yafungua kesi dhidi ya Felix Mosha...soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Dar es salaam
Kampuni ya Uwekezaji ya Nicol imefungua kesi ya madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya Nicol, Felix Mosha na aliyekuwa Mtendaji Mkuu (CEO,Kathleen Armstrong.

Kesi hiyo ya madai namba 282 ya 2017 inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respius Mwijage, ambapo  upande wa wadaiwa umetakiwa  kupeleka utetezi wao, Desemba 20,2017 na kesi hiyo imepangwa kutajwa Januari 24,2018.

Kwa mujibu wa kesi hiyo, upande wa wadai, wanaiomba mahakama hiyo, iamuru wadaiwa hao walipe kiasi cha Sh 180,096,097 kama gharama za hasara walizoingia.

Pia wanaomba mahakama iamuru warejeshe magari, walipe riba ya asilimia 26% pamoja na gharama za kesi.

Katika kesi hiyo, akina Mosha ambao ni wadaiwa wanatetewa na Wakili Hurbet Nyange huku Nicol ambaye ni mdai anawakilishwa na Wakili Benjamin Mwakagamba kutoka kampuni ya uwakili ya BM.

Kwa mujibu wa kesi hiyo inadaiwa kuwa Mosha pamoja na kuondolewa uenyekiti  na wanahisa mnamo mwaka 2012, lakini bado ameshindwa kukabidhi gari  la ofisi aina ya Landcruiser namba T 133 AVG ambapo ilipelekea ofisi ya Nicol kutafuta usafiri mwingine.

Kwa upande wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Kathleen Armstrong  yeye anadaiwa  kwamba akiwa amesimamishwa  na baada ya kuondolewa  na wanahisa,  alishiriki katika kutapanya mali za Nicol ikiwamo kuuza gari aina ya Mitsubish Center Fuso bila idhini ya bodi ama Wanahisa .
Mahakama imeagiza mdaiwa wa pili katika kesi hiyo, Kathleen Armstrong  ambaye ni raia wa Marekani apelekewe notisi  kwa njia sahihi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search