Wataalam wasema afya ya akili tatizo nchini....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es salaam
TAFITI zinaonesha katika kila watu wanne Duniani mmoja anauwezekano
wakupata changamoto ya afya ya akili.
Daktari bingwa wa afya ya akili kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Saidi Luganda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Daktari
bingwa wa afya ya akili kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Saidi Lunganda
akizungumza na waandishi wa habari.
“Tunaposema changamoto ya afya ya akili huyu mtu si mgonjwa,
maana yake kuna jambo limemtatiza,
unaweza ukawa na ugonvi na mwenzako ukapata msongo wa mawazo,” amesema Luganda.
“Msongo wa mawazo unavyokuendesha ndiyo unaweza kusababisha uwezekano
wa kupata matatizo ya kiakili,” ameongeza .
Luganda ametaja baadhi ya sababu za kimaisha zinazoweza
kuchangia kupata matatizo ya afya ya akili ambayo ni kufiwa, kuongezwa cheo,
kuoa na kuolewa, kuachwa na kadhalika.
Akizungumzia hali ya tatizo hilo nchini, amesema ni mbaya na
kueleza kuwa wamekuwa wakiwapokea hospitalini wale tu ambao wanaonekana wazi
kuathirika huku waliowengi na ambao hawaonekani wakishidwa kuripoti vituo vya
afya kwa kuhofia unyanyapaa.
Amebainisha kuwa mara nyingi afya ya akili inapoathirika na
mambo mengine katika maisha huathirika.
Amesema ili kukabiliana na hali hiyo jamii inatakiwa
kuelimishwa na kujua athari zinazoweza kutokea kutokana na tatizo hilo ili hatua
madhubuti zichukuliwe pindi mtu anapobainika kupatia hali hiyo.
Ameeleza kwamba wengi wenye changamoto hiyo wamekuwa wakipelekwa kwa waganga wa
kienyeji na wengine kwenye maombezi bila kupata ushauri wa madaktari kwa ajili
ya kujua hasa tatizo linalomsumbua mgonjwa.
No comments:
Post a Comment