UTAFITI : Watu 9 uambukizwa virusi vya ukimwi kwa siku...soma habari kamili na matukio360..#share


Na Salha Mohamed

MATOKEO  ya utafiti wa viashiria  na matokeo ya Ukimwi (THIS) yameonesha watu 200 huambukizwa virusi vya ukimwi kwa siku nchini.


Waziri wa Afya,Jinsia na Maendeleo ya Jamii, Ummy Mwalimu

Utafiti huo ni kwa kipindi cha mwaka 2016/2017. umefafanua kuwa watu 9  wanaambukizwa virusi vya ukimwi kwa saa.

Taarifa hiyo inasema maambukizi mapya yapo zaidi kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 25-34 kwa asilimia 0.7.

Mbali na utafiti huo kuonesha Tanzania imepiga hatua katika kupambana na ukimwi lakini bado kuna changamoto katika kupambana na kumkinga mtoto asipate maambukizi kutoka kwa mama yake katika kundi la wanawake walio katika umri wa kuzaa.

Tafiti hiyo inaonesha kiwango cha maambukizi kwa watu wenye umri wa miaka 20 hadi 24 kuwa ni makubwa kwa  kundi la vijana hasa wasichana kuwa na maambukizi mara mbili ya maabukizi ya wanaume.

Kutokana na hali hiyo, utafiti huo umebainisha kuwa maambukizi hayo ni hatarishi hivyo kuhitaji ubunifu katika kukabiliana na maambukizi mapya kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 20.

Matokeo hayo pia yameonesha ukubwa wa maambukizi ya kaswende na homa ya ini aina ya B, kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi.


Asilimia 5.6 ya watanzania ya watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi wamewahi kuugua kaswende.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search