Polisi Dar yatoa dakika 15 mkesha mwaka mpya...soma habari kamili na matukio360..#share

Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa dakika 15 kwa viwanja vya Tanganyika Peckers na dakika tano kwenye hoteli maalumu, wananchi kutumia muda huo  kupiga fataki siku ya mkesha wa mwaka mpya  2018.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa.

Pia limepiga marufuku uchomaji wa matairi barabarani kwa ajili ya usalama wa watumiaji wengine wa vyombo vya moto.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es salaam na Kamanda wa polisi wa Kanda hiyo SACP Lazaro Mambosasa alipokuwa akitoa takwimu za uhalifu na usalama barabarani kwa 2016/2017 mbele ya waandishi wa habari, amesema watakaokiuka watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Mwaka huu tungependa kusherehekea kwa namna tofauti tutakuwa pele Tanganyika Peckers kwa watanzania wengine wanaotaka kulipua hizo fataki tutakuwa hapo kuna eneo zuri, tutakuwa tumewaandaa watuna tutawaruhusu watu kufyatua hizo fataki,’’ amesema.

Ameongeza “Maeneo mengine ni ya vibali maalum ambavyo vinatolewa na jeshi la polisi kanda maalum, nazo ni hoteli chache na tumewapa dakika tano tu lakini pale ambapo tumeainisha tutakuwa pale Tanganyika Pechers muda tutatoa kama robo saa kwa ajili ya zoezi hilo,”

Takwimu za uhalifu na usalama barabarani Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam 2016/2017

Amesema kwa kipindi cha kuanzia  Januari hadi Novemba 2017 matukio ya uhalifu yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi kanda hiyo  ni 126,200 ukilinganisha na kipindi kama hicho 2016  ambacho kilikua na matukio 129,602 hivyo kusababisha upungufu wa matukio 3,405 sawa na asilimia 2.6.

Pia amesema Katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2017 kulikua na jumla ya matukio makubwa ya jinai 9,736 ukilinganisha na matukio makubwa ya jinai 12,550 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho 2016 na upungufu wa matukio 2,814 sawa na asilimia 22.4 na hali ya uhalifu ilikuwa ya kuridhisha ingawa kulikuwa na matukio machache ya unyang’anyi wa kutumia silaha, unyang’anyi wa kutumia nguvu, uvunjaji, wizi wa magari na pikipiki yaliyojitokeza.

Mpango  mkakati  wa kuzuia uharifu mwaka 2018

SACP Mambosasa amesema miongoni mwa mikakti waliyopanga kufanya katika juhudi za kupunguza uhalifu mwaka ujao ni kutumia  falsafa  ya  Polisi  Jamii,kwa jeshi hilo kuwa  karibu zaidi na wananchi  ili kuweza  kupata  taarifa  zaidi  kuhusu  mbinu za  uhalifu na wahalifu.

kufanya doria/misako na oparesheni  maalum katika  maeneo  mbalimbali, doria za miguu, Magari, Pikipiki na Mbwa na Farasi.

Kuimarisha vikosi kazi (Task Force) ngazi ya wilaya na mkoa pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Kuimarisha  kikosi cha kupambana  na  wezi  wa  magari  hususani maeneo ya pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.

Kuendelea kushirikiana na mikoa jirani kwa kubadilishana taarifa za kiintelijensia  na  kufanya  oparesheni za  pamoja.


Kamanda huyo ameomba jeshi hilo kupatiwa ushirikiano na wananchi ili kuzuia na kupunguza uhalifu katika kipindi cha mwaka 2018.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search