Zitto Kabwe amvaa rais Magufuli...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

KIONGOZI mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemuomba rais John Magufuli kuweka tangazo lake wazi kwa umma la rasilimali na madeni alilowasilisha  jana.


Kauli ya Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma mjini inafuatia jana rais Magufuli kuwasilisha fomu  yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam.


Zitto Kabwe

Leo katika ukurasa wake wa Twitter, Zitto ameandika: "Mmemwomba Rais aweke hilo tangazo lake wazi? Nadhani vyombo vya Habari mwende zaidi ya kuripoti ( kwa miaka zaidi ya 20 amekuwa akijaza fomu kama Waziri na baadaye Rais na pia wenzake waliomtangulia ). Twende hatua ya mbele zaidi, Mali hizi ziwekwe wazi na umma uchambue."


Jana baada ya kuwasilisha fomu hiyo rais Magufuli aliipongeza sekretarieti hiyo kwa kazi inazofanya na kumtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017.

“Mhe. Jaji Nsekela ikifika tarehe 31 Desemba, ambayo ni siku ya mwisho kwa Mujibu wa sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema,” alisisitiza  rais Magufuli.

Kwa upande wake Nsekela alimshukuru na kumpongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu kujaza fomu hizo na amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi wa umma siyo ombi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search