Tundu Lissu akaa kwa mara ya kwanza...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

HALI  ya kiafya ya mwanasheria mkuu wa chama cha Chadema, Tundu Lissu inaendelea kuimarika na sasa ameanza kukaa mwenyewe.

Hatua hiyo ni muendelezo wa kuimarika kwa afya yake,Disemba 26,2017 alitangaza kusimama kwa msaada wa wahudumu wa hospitali  Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi mwezi Septemba mjini Dodoma.


Tundu Lissu

Leo katika ukurasa wake wa Instagram Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashirika ameandika:

"Ninawashukuru kwa sala na maombi yenu. Sasa ninaweza kukaa bila ya kuegemea kitu!!!"

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search