Rekodi mpya ya ufungaji magoli yawekwa EPL...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mashirika ya kimataifa
Harry Kane amefunga hat-trick na  kuweka rekodi mpya ya mabao mengi yaliofungwa kwa mwaka 2017 huku Tottenham ikiicharaza Southampton  5 -2 katika uwanja wa Wembley.
Harry Kane wa Tottenham akifunga moja ya goli katika mechi dhidi ya Southampton
Mshambuliaji huyo wa Spurs na Uingereza alifunga bao lake la 37 la mwaka 2017 katika dakika ya 22 na  kuipiku rekodi ya Alan Shearer iliowekwa wakati alipokuwa akiichezea Blackburn 1995.
Kane baadaye aliongeza mabao mengine mawili katika vipindi vyote viwili na kufanya jumla ya mbao aliyofunga kwa klabu na taifa kuwa 56 mawili zaidi ya mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi.
Kabla ya bao la tatu la Kane, Dele Alli alikuwa amefanya matokeo kuwa 3-0 katika dakika ya 49 wakati alipocheka na wavu na dakika mbili baadaye akampatia Son Heung-min ambaye alimfunga kipa Fraser Forster.
Southampton ikicheza bila mfungaji wake mkuu Charlie Austin ilijipatia bao lake la kwanza kabla ya Dusan Tadic kuongeza la pili.
Licha ya kuimarika katika kipindi cha pili , Southampton haikuweza kuharibu sherehe ya Tottenham na sasa wamecheza miezi miwili bila ushindi.
Wakati huohuo Spurs imeipiku Liverpool katika nafasi ya nne huku The Reds wakicheza dhidi ya Swansea siku ya Jumanne.
Akizungumza kuhusu rekodi yake ya miaka 22 iliyovunjwa, Shearer alituma ujumbe wa Twitter akisema: Umekuwa na mwaka mzuri sana wa 2017 .Unahitaji kuchukua rekodi hiyo ya mabao mengi katika ligi ya uingereza katika mwaka mmoja . Kongole na enedelea na kazi nzuri.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search